Habari msomaji wa makala hizi za uhifadhi wa wanyamapori, karibu katika makala ya leo, tukumbushane kidogo kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa maliasili zetu. Kama wengi wetu tunavyofahamu nchi yetu Tanzania ina utajiri mkubwa sana wa maliasili za wanyamapori na mimea asilia, ambayo inahitaji uangalifu mkubwa sana ili iweze kuendelea kuwepo kwa sababu ya umuhimu wake katika mfumo wetu wa maisha.

Wanyama na mimiea ni sehemu muhimu sana ya mfumo wa maisha yetu hapa duniani, kwasababu kama alivyoumba Mungu, tunategemeana kwa kiasi kikubwa sana katika mazingira tunayoishi, binadamu anategemea mimea kuishi, wanyama wanategemea mimea kuishi, lakini pia kuna wanyama wengine wanategemea wanayama wenzao kuishi maisha yao, pia hata mimea inategemea uwepo wa wanyama kuishi.

Hivyo basi uhifadhi wa maliasili ni jambo muhimu sana katika maisha yetu, kwa sababu nyingi za kimaisha na kimazingira, uhifadhi unatuhitaji sisi sote kuhakikisha unaendelea kuwepo kwa ajili ya kuboresha maisha ya wanayma na mimiea. Kama kimojawapo kitakosekana basi mfumo mzima wa maisha hautakwenda sawa, na majanga mengi yatatokea duniani na kutusababishia madhara makubwa.

Katika nchi yetu Tanzania, uhifadhi unatakiwa upewe kipaumbele sana kwa sababu kwanza nchi yetu imetenga maeneo mengi na makubwa kwa ajili ya uhifdhi wa wanayamapori na misitu, maeneo ya misitu ya pwani na maeneo mengine serikali ya Tanzania imeyatungia sheria za uhifadhi wake na inamtaka kila mtanzania awajibike katika uhifadhi wa maliasili hizi muhimu.

Nawaomba na kuwasihi watanzania wenzangu mnaosoma makala hii, kutambua umuhimu huu wa maliasili zetu na kuzitunza pia kutoa ushirikiano kwa mamlaka za uhifdhi sehemu yoyote ile uliopo. Uhifadhi wa maliasili unaanzaia hapo ulipo kwenye mazingira yanayokuzunguka. Kwa mfano angalia mazingira yanayokuzunguka yapo safi, una utaratibu wowote wa kupanda miti au kushiriki katika kampeni za upandaji miti? Utunzaji mzuri wa taka za aina zote nk.

Kwa kushiriki katika kuweka mazingira yetu safi tutakuwa tumesaidia sana kuokoa maelfu ya viumbe hai wengine wanaokufa kila siku kwa sababu ya utaratibu wetu wa maisha ambao hauzingatii usafi wa mazingira. Mazingra yetu yasipokuwa safi athari zake zitaenda hadi kwenye maliasili nyingine muhimu.

Naamini nitakuwa nimekukumbusha jambo moja muhimu kwenye makala hii, naamini pia utayafanyia kazi yote tuliyokumbushana kwenye makala hii. Nakutakia kila la heri katika kufanikisha haya tuliojifunza leo katika makala hii.

Ahsante sana!

Hillary Mrosso

255 683 862 481

hillarymrosso@rocketmail.com