Jitihda na juhudi za kila serikali duniani ni kuhakikisha maisha ya binadamu yanaendelea kuwa bora kwa kuhakikisha kila kinachotishia uhai na maendeleo ya binadamu kinachukuliwa kwa uzito wake bila kujali tofauti zilizopo za kisiasa, kiuchumi, kidini au kwa namna yoyote ile, linapokuja suala la kuyafanya maisha ya binadamu yawe bora na yaendelee kuwepo kwa miaka mingi lazima viangaliwe viatarishi na vitu vyote vinavyochangia hatari hii ya maisha ya binadamu juu ya uso wa nchi. Vipo viatarishi vingi sana kama vile magonjwa yasiyotibika kama vile UKIMWI, kansa na magojwa mengine makubwa yanayotishia maisha ya binadamu hapa duniani. Lakini hapa kuna kiashiria kibaya sana kinacho enea kwa kasi baadhi ya sehemu na sehemu nyingine kwa haraka sana, hii ni UHARIBIFU WA MAZINGIRA.
Nchi yetu ya Tanzania bado inamaeneo mengi sana yaliyobaki na uhalisia wake, hapa namaanisha kuna maeneo mengi ambayo hakuna uharibifu mkubwa unaosababishwa na shughuli za kibinadamu. Hivyo hii ni nafasi nzuri naya pekee kwetu kuwa na sera madhubuti sana ambazo zitaeleza moja kwa moja kuwa maeneo fulani yanahitaji uangalizi wa kina na haruhusiwi mtu yeyote kuhusika kwa namna moja ama nyingine kwenye kukata au kufanya shughuli yoyote ndani ya maeneo hayo. Misitu tuliyonayo ituzwe sana, mapori tuliyonayo yatunzwe sana, mabonde na milima tuliyonayo itunzwe kweli kweli. Vitu vyenye manufaa ya muda mfupi yasitufanye kuharibu mfumo mzima wa ikologia ya asili inayoleta faida kubwa kwa maisha ya binadamu na wanyama.
Janga kubwa tulilio nalo sasa ni janga la uharibifu wa mazingira, kila sehemu duniani wanalia kuhusu utunzaji wa mazingira, nchi nyingi zinzkaa vikao na mikutano mingi na mikubwa inafanyika kila siku ili kunusuru hali mbaya ya uharibifu wa mazingira inayoshamiri kila kona ya dunia. Katika kukaa na kutafakari hadi kufikia hatua hii ya kuandika makala hii, nimefikiri na natamani kila mtanzania awajibike kwenye hili la mazingira. Suala la utunzaji na uhifadhi wa mazingira lisiwe ni jambo linalongoja tarehe maalumu au siku maalumu, linatakiwa kuwa ni suala la kila siku ili maisha yetu yaendelee kuwepo hapa duniani. Jinsi tuanavyjitunza sisi wenyewe kwa uangalifu mkubwa ili tuendelee kuwepo na kuendelea kuishi ndivyo tunavyotakiwa kuyachukulia hivyo mazingira yetu yanayotuzunguka.
Kwa nchi zetu huku Afrika ambazo kwa kiwango kikubwa zinategemea kilimo , zinaweza kuadhirika zaidi kutokana na kutokuwa na vyanzo vingine mbadala vya uzalishaji, hivyo kuharibika kwa mazingira ni tishio kubwa sana kwenye usalama wa chakula kwa nchi hizi za Afrika kwa siku za usoni, kila tunacho kitegemea kitashindwa kutusaidia endapo tutaitumia leo vibaya kwa kuharibu mazingira ambayo Mungu ameyaweka yatusaidie. Kuna usemi maarufu sana unaosema “tunza mazingira yakutunze” msemo huu una ukweli mtupu sana ndani yake kwani hakuna anayeweza kuendesha maisha yake kwenye ardhi isiyo na rutuba au jangwani. Kila mtu anahitaji mazingira mazuri yanayozalisha ili kuendesha maisha yake. Hivyo basi tunza mazingira yakutunze.
Kuna wanaofikiri mawazo ya kibinafsi bila kufikiria vizazi vijavyo, watu wanaharibu mazingira kwa makusudi kabisa, watu wanafanya ujangili kwa makusudi kabisa, watu wanaharibu vyanzo vyamaji kwa makusudi kabisa, wnafanya hivi kwa kuwa hawana maono ya mbali yenye msaada kwa vizazi vijavyo. Wanajifikiria wao tu, wanaangalio wao wakishiba tu basi, hawajali tena.
Kama hatutaamka na kupambana kwenye hili la utunzaji wa mazingira, mambo yanayotegemewa na kutabiriwa siku zijazo kwa bara la afrika hasa ni mabaya. Hii ni kutokanana na sababu nyingi sana Afrika inakabiliwa na changamoto hii ya utunzaji wa mazingira. Ongezeko la watu kupita kiasi, mifumo ya kiuchumi, siasa na maendeleo ya teknologia nyingi za kisasa ambazo kwa asilimia kubwa zita waacha Waafrika wengi mbali na namna ya kupata kipato kwa maendeleo haya hivyo kuona nafasi walionayo na wanayoiweza ni kuhamia kwenye rasilimali za misitu na maeneo muhimu yaliyohifadhiwa, vyanzo vya maji hivyo shughuli za kibinadamu zitashamiri sana kwenye sehemu zilizotengwa kutokana na ukosefu wa ajira na kuongezaka kwa uzalishaji.
Mwisho, naipongeza sana serikali hasa ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia mazingira kwa kuungana na dunia nzima kuhakikisha dunia inakuwa sehemu salama ya kuishi, vile vile kwa dhamira na juhudi za dhati na za makusudi zinazoonekana kwenye utunzaji wa mazingira. Napenda wadau wote wa mazingira tuungane na tuunganishe nguvu pamoja na kuwa na mfumo mzuri unaowafanya watu na jamii nzima kushiriki kikamilifu kwenye hili la uhifadi wa mazingira yetu. Najua kuna mambo yanayoweza kutugawa kulingana na tofauti zetu lakini kwenye hili tu la mazingira lituunganishe na kushirikiana kwa pamoja bila kujali misimamo na itikadi zetu. Hali ya ukame na matokeo ya uharibifu wa mazingira haitasimama upande mmoja tu wala kuwa kama itikadi zetu zilivyo bali itatuathiri sote, na hata watoto, wajukuu wetu. Hivyo ndugu mtanzania mwenzangu tuwajibike isije watoto na wajukuu wetu wakaja kusema mazingira haya yameharibika kwa sababu ya wazee au wazazi wetu,au viongozi wetu walishindwa kuwajibika kwenye utunzaji wa mazingira.
Hillary Mrosso
0742092569