Habari msomaji wa mtandao wetu wa wildlife Tanzania, hongera tena kwa siku nyingine mpya katika mwaka huu wa 2018, naamini umeupokea vizuri na umejipanga vizuri kufanya mambo makubwa na bora sana kwako na kwa familia yako au jamii yako. Karibu kwenye makala ya leo ambayo natamani kuzungumzia jambo moja linalohusu uwepo wa biashara halali ya meno ya tembo. Kwenye makala niliyoandika jana nilielezea tukio kubwa la kihistoria ambalo lilikuwa linasubiriwa kwa shauku na maelfu ya watafiti, wahifadhi na wapenzi wa wanyamapori na uhifadhi. Nilielezea maamuzi ya nchi ya China iliyofanya katika siku ya mwisho ya mwaka 2017.

SoMA MAKALA HII; Tumaini Kubwa Kwa Tembo Wa Afrika

Kutokana na taarifa mabali mbali zinazoelezea ujangili na masoko ya biashara ya meno ya tembo huko China, na kupitia taarifa kwenye mitandao ya google, kwenye gazeti maarufu la National Geographic na the Gudiani inaonyesha badhi ya maoni ya watu waliyokuwa nayo baada ya kufungwa kwa masoko ya biashara ya meno ya tembo huko China. Ni jambo kubwa sana na la maana sana kwa nchi ya China kufikia uamuzi huu wa kufunga masoko yake na viwanda vya kutengenezea bidhaa mbali mbali zitokananzo na meno ya tembo. Naamini kabisa kama wanavyaomini wahifadhi wenzangu na watu wengine jambo lililofanywa na China kufunga masoko yake itasaidia sana kupunguza au kuondoa ujangili wa tembo. Wachambuzi wa mambo wanasema tangu China itangaze kufunga masoko na biashara ya hiyo ya meno ya tembo mwanzoni mwa mwaka 2017, mauzo ya meno ya tembo yameshuka kwa 65% hii ni kiwango kikubwa sana cha anguko la soko kwenye biashara hii.

Kwa hatua za mbele zilizochukuliwa na China kuharibu na kuzuia biashara hii ni faraja kubwa sana kwa wadau wa wanyamapori na wahifadhi ambao walilivalia njuga jambo hili kwa miaka mingi. Na kama kwa kutangaza kuwa haitaendesha tena biashara hii na mauzo yameshuka kwa kiwango hiki, inamaanisha hatua nyingine za maisha kwa waliokuwa wanategemea biashara hii kuedesha maisha yao zimefanyika. Kwa namna hii ni kwamba biashara hii sasa haina mvuto wa aina yoyote kwenye nchi ambazo zilikuwa zinahitaji meno ya tembo, hivyo hata kwa wale majangili na watu wanaingia hatari ya kupoteza maisha yao kwasbabu ya kwenda kufanya ujangili wa tembo, hamu na hamasa ya kuendelea na vitendo hivi itapungua kama sio kuondoka kabisa.

Aidha licha ya kwamba China imefunga masoko yake makubwa ya biashara hiyo ya maeno ya tembo, lakini tafiti zinaonyesha haijafunga kila kitu au kuzuia kabisa biashara hii kwenye nchi yao. Kumebakia na maeneo machache sana ambayo yanasimamiwa kwa makini. Tafiti za ndani ya China kwa watengenezaji wa bidhaa zitokanazo na meno ya tembo walisema kuwa wanataka tembo wahifadhiwe na kwamba wao hawaitaji meno mengi ya tembo kwa ajilia ya kazi zao, wamesema wao wanahitaji meno machache sana, mmoja ameripotiwa akisema tembo wanaokufa kwa umri mkubwa au kwa majanga ya kiasili meno yao yanatosha sana kwa shughuli yao, hivyo hawahitaji tembo wauliwe na kuwindwa kwa ajili ya meno ya ziada.

Kwa wahifadhi na wafuatiliaji wa masuala haya hili ni jambo ambalo tunatakiwa kulifikiria na kulichambua ili kuhakikisha hata kama kuna kiasi kidogo sana cha biashara hii kinaendelea basi kifanyike kwa weledi na kwa nidhamu ya hali ya juu sana. Na pia watafiti wa mambo haya wa muda murefu wamekuwa na wasiwasi kwenye namna ya utekelezaji wa biashara ya utalii wa uwindaji ambao hufanyika sana kwa sababu mbali mbali, utalii wa uwindaji au uwindaji wa wanyamapori kihalali unaweza kuwa ni kama njia au mlango wa kuendelea kwa uwindaji haramu chini yake. Hivyo wamekuwa na mawazo mengi sana. Na wengine walipenda kabisa kusimamisha au kutoruhusu biashara ya uwindaji halali kwenye maeneo ya hifadhi za wanyamapori.

Wasiwasi wao ni kwamba endapo uwepo wa uwindaji kihalali utaruhusiwa kwenye hifadhi zetu, mambo mengi yanaweza kufanyika nyuma ya pazia ambapo hakuna mtu anawyeweza kutambua jambo hili mapema hivyo, wamekua na wasiwasi kwenye eneo hili la uwindaji na kushauri endapo litaendelea kufanyika basi lifanyike kwa umakini na usimamizi wa karibu.

Naamini umepata mambo machache ya kukusaidia kwenye uelewa wako kuhusu biashara hii na mitazamo ya watu mbali mbali kwenye utekelezaji wa maazimio mbali mbali. Asante kwa kusoma makala hii nakutakia mafanikio na heri yam waka mpya 2018.

Ahsante sana

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 862 481/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania