Habari mtanzania mwenzangu, hongera kwa siku ya leo. Leo ni siku ya kipekee ambayo tunakwenda kuangalia baadhi ya mambo muhimu kwenye utalii wetu na kwenye maliasili zetu. Hivyo karibu tuone mambo mbali mbali na vivutio mbali mbali vilivyopo hapa duniani. Ni baadhi ya maneno ambayo nimekuwa nikayatumia sana kwenye uandishi wa makala za wildlife Tanzania, hivyo nimeyaelezea maneno haya kwa ufupi ili upate picha kubwa ninayotaka uione kwenye makala na maliasili zetu za Tanzania. Hivyo karibu fuatana nami kwenye makala hii.
Mtalii
- Ni mtu anaye safari na kwenda nje ya mahali alipokuwa mwanzo
- Ni mtu anayesafiri kwenda kwenda kwenye mazingira tofauti na aliyozoea
- Ni kwenda maeneo kutembelea maeneo ya vivutio kwa muda usiozidi mwaka mmoja
- Ni mtu anayesafiri kwenda mbali na mazingira ya nyumbani kwa sababu mbali mbali, kama vile starehe, biashara, au sababu nyingine.
Vivutio
- Ni kitu kinachofurahisha na kusisimua
- Ni kitu kinachoteka na kukufanya ushangae
- Ni sehemu inayovutia na kushawishi watu kwenda kutembelea
- Ni vitu au kitu ambacho ni kigeni ambacho kila mtu anavutika kukiangalia
- Ni vitu ambavyo huwafanya watu wasafiri kuona vitu hivyo
Vivutio vya Kitalii
- Ni vitu ambavyo vinavyofanya watu wasafiri kuona vitu hivyo
- Ni sehemu yenye maajabu ambayo kila mtu anatamani kuviona
- Vitu hivi vinaweza kuwa;
- Utamaduni
- Hali ya hewa
- Asili
- Uoto wa asili
- Makumbusho
- Sehemu za kihistoria
- Sehemu zenye miji mikubwa
- Maporomoko ya maji
- Majangwani
- Misitu minene
- Mbuga za wanyama
- Wanyamapori waliofugwa (zoos)
- Bahari
- Mito
- Mabwawa ya maji
- Maeneo oevu
- Maeneo yenye viwanda na mitambo mikubwa
- Milima na miinuko
- Tambarare zenye nyasi na mchanga
- Fukwe za bahari
- Kwenye maonyesho mbali mbali
- Kwenye visiwa mbali mbali
- Sehemu zenye mashamba makubwa
- Sehemu zenye mawe na miamba
- Sehemu zenye miti mikubwa yenye mapango
- Sehemu zenye ndege wengi
- Maeneo yenye mahoteli makubwa
- Maeneo yenye biashara sana
Kuna maeneo mengi sana ya kutembelea kwa hapa Tanzania na duniani kwa ujumla, hivyo elewa nini kinakuvutia zaidi na jipange kwenda kutembelea, nenda katembelee, nenda tu sio tu kwamba utaburudika na kufurahia bali utajifunza sana mbinu mbali mbali za maisha na maisha yako yatakuwa bora.
Kuna maeneo mengi sana hapa nchini yametengwa kwa ajili ya viumbe hai na maliasili nyingine muhimu sana. Mengine yanalindwa na sharia kali sana kwa sababu ya umuhimu wake kwenye ikologia ya viumbe hai. Hivyo nimeainisha baadhi ya maeneo ambayo yanawafanya watu wengi kuvutika na kupanga safari kutembelea maeneo hayo.
Hillary Mrosso
Wildlife conservationist
0742092569/0683248681
htt://www.mtalaamu.net/wildlifetanzania