Habari njema kwa wasomaji na wafuatiliaji wa mtandao wetu wa wildlife Tanzania.

Tangu tuanze uandishi wa makala za wanyamapori mwaka 2017, hatujawahi kuwa na logo rasmi inayotutambulisha.

Lakini sasa tunapenda kuwajulisha logo mpya ambayo itakaa katika blogu yetu na kwenye vitu mbali mbali tutakavyovitengeneza.

Logo hii utambulisho wetu rasmi, na tunayofuraha endapo itatumika kuwakilisha kile tunachokifanya katika kazi yetu ya kuelimisha jamii kuhusu Maliasili zetu.

Kuanzia sasa hii ndio itakuwa logo yetu katika vitu mbali mbali ambavyo tutakuwa tunavifanya, kwenye uandishi wa makala, tisheti, mashati, vikombe na bidhaa nyingine zote zitakuwa na logo ya wildlife Tanzania.

Ukiangalia hiyo logo utaona rangi mbali mbali na muundo wa herufu ‘W’ ambayo imesimama badala ya wildlife au viumbe hai wote wa wituni, wanyama na mimea.

Lakini, ukiangalia kwa makini kwenye hiyo nembo yetu, utaona kama mapembe ya wanyama jamii ya swala, ikiwa na maana ya kuwakilisha wanyamapori wote.

Kwa ufupi tunayofuraha kukujulisha wewe msomaji na mfuatiliaji wa makala zetu kuhusu uwepo wa logo yetu mpya tutakayoitumia.

Karibu sana tuzidi kushirikiana na kujulishana mengi kuhusu uhifadhi, wanyamapori, mazingira na utalii.

Hillary Mrosso

you might also like