Habari rafiki, naamini unaendelea vizuri na mapambano ya maisha ya kila siku, leo tutajifunza samari ya mambo yote tuliojifunza kutoka katika sehemu ya tisa ya sheria hii. Hii ni sehemu ya sheria isiyo na vipengele vingi, bali inavipengele vitatu tu. Hivyo kwa kuandika makala hii itasaidia sana kwenye uelewa wa vipengele na mambo ya msingi yaliyoelezewa kwenye kila kipengele. Karibu sana.
Kwenye sehemu hii ya sheria kuna vipengele nitavielezea ili sheria hii ieleweke vizuri na wengi. Kama unavyojua tuanchambua sehemu ya tisa ya sheria ya uhifdhi wa wanyamapori Tanzania. Kuna mengi ya kujifunza na kufanyia kazi kwenye sehemu hii ya sheria ya wanyamapori.
1.Ufafanuzi na tafsiri (Interpretation)
Kwenye kifungu cha 77 cha sehemu hii ya sheria kinaelezea maana na tafsiri ya maneno yaliyotumika hapa, kwa mfano maneno kama nyara yamaelezewa vizuri sana kwa mujibu wa sheria hii. Nyara kwa tafsiri ya kifungu cha 77 ni meno ya ndovu, pembe za faru, meno ya kiboko, Ngozi za wanyama, pembe za wanyama; na kwa upande mwingine sheria imetoa maana ya nyara zilizotengenezwa (manufactured trophy) ikiwa na maana ya kitu chochote kilichotengenezwa na meno, mifupa, kucha, kwato nywele au manyoya mayai au sehemu yoyote ya mnyama yoyote. Hivyo kifungu hiki kimeelezea na kutoa mwongozo kwa maneno yatakayotumika yatakayotumika kwenye sehemu hii ya sheria ya wanyamapori.
2.Uwasilishwaji wa Nyara kwa ofisa ndani ya siku thelatini (Trophy to be produced to the licenced officer within thirty days)
Kwenye kifungu hiki cha sheria ya wanyamapori kinaelezea utaratibu wa kufuata wakati wa kutoa nyara, vibali, silaha na maeneo ambayo nyara za wanyama zimepatikana. Pia usajili wa nyara unatakiwa utolewe uamuzi wa Waziri kwa mujibu wa kanuni.
- 3. Makosa kuhusiana na wasio na usajili (Offences relating to non- registration)
Kifungu cha 79 kinaelezea utaratibu wa kuhamisha au kupeana nyara kwa kwa mtu mwingine. Hapa kinaelezea makosa na adhabu ya watu wanaokiuka utaratibu wa uvunaji wa nyara.
Naamini katiaka sehemu hii ya sheria inaelezea vipengele vyote vitatu vya sehemu hii ya sheria vinavyoelezea masuala yote ya yaliyoelezwa vizuri zaidi.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania