Tembo wa Afrika (Loxodonta Africana), ndiye mnyama mkubwa kuliko wote waishio nchi kavu. Mnyama huyu ni jamii ya wanyama walao majani (herbivores). Tembo hawa hupatikani nchi za kusini mwa jangwa la Saharara pamoja na Afrika.
Yafahamu haya kuhusu tembo wa Afrika.
- Masikio ya tembo hawa yamefanana sana na raman ya bara la Afrika hivyo kupelekea tembo hawa kupewa jina la tembo wa Afrika.
2.Meno ya tembo huweza kutoa makadrio ya umri wa tembo husika.
Hii ni kwa sababu meno hayo hukua sambamba na umri wa tembo hivyo, hivyo ukubwa wa meno hueleza umri wa tembo huyo.
3.Tembo hutumia masaa 12-18 wakila majani na mimea, na inakdiriwa kuwa tembo hulala kwa masaa mawili tu wakati wa usiku pale anapokuwa kwenye mazingira yake asilia.
- Tembo jike hubeba mimba kwa muda wa miezi 22, na mtoto tembo anapozaliwa hupewa matunzo kutoka kwa mama yake akishirikiana na tembo wote waliopo kwenye kundi husika, mtoto huyo hunyonya kwa muda wa miaka 3- 4, na ana uwezo kunyonya maziwa hadi galloni tano kwa siku kutoka kwa mama yake.
5.Tembo anaweza kuishi na kufikia miaka 60- 70 asipouriwa na binadamu.
6.Tembo jike ana uwezo wa kuzaa watoto wasiozidi watano katika maisha yake yote.
7.Tembo ana uoni hafifu lakini ana uwezo mkubwa wa kunusa na kutambua harufu. Tembo wote huzaliwa wakiwa vipofu.
8.Kidunia tembo wanonekana kuishi katika mazingira hatarishi ambayo yanaweza kupelekea kutoweka kwako, ugumu huu husababishwaba na:
-Biashara ya pembe za ndovu.
-Migogoro kati ya binadamu na tembo.
-Uharibifu wa makazi ya tembo.
- Nini kifanyike ili kuwanuauru tembo wa Afrika.
-Tuiipinge na hatimaye kuitokomeza biaahara ya pembe za ndovu.
– Tuziunge mkono jitahada za uhifadhi wa wanyamapori.
-Tushiriki kikamilifu katika kutoka elimu ya umuhimu wa wanyama pori na athari za ujangili.
MIMI NAWAPENDA TEMBO, NITAWALINDA NA KUWATUNZA, WEWE JE?
Ahsante sana!
Lucy Romward