Habari msomaji wa Wildlife Tanzania, karibu kwenye makala ya leo ambayo tutajifunza kwa pamoja mambo yote tuliyoyachambua ndani ya sehemu hii ya saba ya sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009. Hii ni sehemu nzuri sana na yenye vipengele vingi vinavyohusu, uwindaji, matumizi ya wanyamapori na utalii wa picha au utalii usiohusisha uwindaji wa wanyamapori. Hivyo makala ya leo nimeiandaa kwa ajili ya samari ya sehemu hii ya saba. Hivyo fuatana name kwa mengi zaidi.
- 1. Kamati ya Ushauri wa Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji (Hunting Block Allocation Advisory Committee and procedure on application)
Inaanzia kifungu cha 38 chote, ambacho kinaelezea kanuni zote za kisheria za uwindaji na kupata lesseni.Hiki ni kipengele ambacho kinahusu vitalu vya uwindaji kwa ujumla, masharti na kanuni za uwindaji kamati za ushauri kuhusu maswala ya uwindaji, majukumu ya Waziri kwenye haya maswala, majukumu ya Mkurugrnzi na matakwa ya sheria ya uwindaji. Ushauri kuhusu mambo ya uwindaji na adhabu ya kifungo au kulipa faini endapo mtu atakukiuka masharti ya uwindaji na kanuni zake. Ni kipengele kizuri sana kwa kufahamu njia zote za msingi kwenye uwindaji wa wanyamapori.
2.Waziri anaweza kuzuia utolewaji wa lesseni na vibali (Minister may restrict grant of licenses and permits)
Sehemu hii ya kipengele hiki kinaanzia na kifungu cha 39 chote inaelezea mamlaka ya Waziri kutoa au kuzuia vibali vya aina mbali mbali, kwa wageni na wazawa kwenye sehemu hii yameelezwa vizuri na kwa undani zaidi. Na mashareti yote yahusuyo utolewaji wa lesseni na vibali.
3.Hakuna uwindaji bila lesseni (No hunting without license)
Kipengele hiki kinaanzia kifungu chote cha 40 cha sheria hii kinafafanua na kuelezea masharti na mapendekezo ya sheria ya wanyamapori kwamba uwindaji wowote wa wanyamapori hautafanyika bila kuwa na lesseni au kibali.
4.Kubadilika kwa majedwali (amendments of schedules)
Kwenye sheria hii kifungu chote cha 41 kinaelezea sehemu hii. Kuna majedwali ambayo yamepewa majina mbali mbali ambayo yana wanyamapori wa aina mbali mbali, sheria hii inatoa mwongozo wa namna ya kufanya kwenye kila jedwali. Wanyama kwenye majedwali yote yaliyopo humu yanaweza kubadilishwa na kuwekwa kwenye jedwali jingine. Na mamlaka ya kufanya hivyo anayo Waziri.
5.Kuwajeruhi wanyamapori ( Wounding of animals)
Hiki ni kipengele chote cha kifungu cha 42, kinachoelezea endapo mwindaji amemjeruhi mnyama katika harakati za kumwinda anapaswa kuhakikisha mnyama huyo anamuua na asimwache bila kumuua.
6.Masharti ya jumla kuhusu lesseni za wanyama wa kuwindwa (General provisions relating to game license)
Kifungu chote cha 43 kinaelezea masharti ya uwindaji, lesseni na wanyama wa kuwindwa, hivyo ni sehemu nzuri sana ya kujua mengi kuhusu uwindaji na lesseni sahihi za uwindaji.
7.Nyara na uwindaji wa kujikimu (Trophy and Subsistence hunting)
Kipengele hiki kinaanzia kifungu chote cha 44, ambacho kinaelezea mambo ya kisheria kuhusu nyara na matumizi mengine ya uwindaji. Wanyama wa kuwindwa na pia nyara zote ambazo serikali imejichagulia kuwa ndizo nyara zake.
- Upatikanaji wa wanyamapori kwa ajili ya uwindaji kwa jamii (Access to wildlife by traditional community)
Hiki ni kipengele kinaelezea kifungu chote cha 45, ambacho kinaelekeza na kutoa utaratibu wa jamii kuwa na nafasi ya kuwinda na kutumia wanyamapori kwa mujibu wa sheria.
9.Uwindaji kwa wanyama waliotajwa na waliopo kwenye Jedwali (Hunting Of specified And scheduled animals)
Kifungu chote cha 46, kinaelezea sana mkazo kwa uwindaji wa wanyama walioainishwa na kukubaliwa kuwinda wanyama waliopo kwenye jedwali au waliotajwa, na hapa inaonyesha wanyama wapi wanawindwa, idadi na wanatoka kwenye jedwali gani la sheria hii.
10.Kukiuka masharti ya wanyama ambao umepangiwa kuwawinda kwa mujibu wa sheria (Unlawful hunting of specified or scheduled animal)
Kifungu cha 47 chote kinaeleza, endapo umepangiwa wanyama sahihi wa kuwinda idadi na aina za wanyama lakini ukikiuka masharti ya sehemu hii, hivyo kipengele hiki kinaelezea wanaokiuka au wanaoshindwa kufuata sheria za uwindaji pamoja na adhabu zao.
11.Lesseni ya mtalaamu wa uwindaji (Professional hunter licence)
Sehemu hii yote ya kifungu cha 48, Inaelezea wataalamu ambao wanahusishwa kwenye uwindaji, matumizi ya lesseni zao. Sifa za kuwa na lesseni ya utaalamu wa uwindaji na masharti ya kupata lesseni hii.
12.Lesseni ya mtaalamu wa uwindaji kwa wasio wazawa (Professional hunter licence for a non-citizen)
Kipengele hiki kinaelezea kifungu chote cha 49, kuwa wazawa kumiliki lesseni za utalaamu au ubobezi kwenye mambo ya uwindaji, jinsi inavyofanya kazi kisheria na jinsi inavyotolewa na sheria imeelekeza hata jinsi lesseni hii inavyokosa uhalali wa kufanya kazi kisheria.
13.Hakuna mnyama atakayekamatwa bila kibali (No animal to be
Captured without permit)
Sheria inasisitiza katika kifungu chote cha 50, kuwa hakuna mnyama atakayekamatwa bila kibali kutoka mamlaka husika, na pia sheria inaelekeza makusudi ya ukamataji wa wanyama baada ya kupata kibali, unakamata wanyama kwa lengo gani au kwa nia gani, hapa unaeleza sababu, na kama sababu hazikidhi vigezo kwa mujibu wa sheria basi unaweza kukosa kibali cha kufanya hivyo.
14.Utolewaji wa kibali cha ukamataji (Grant of capture permit )
Kifungu hiki cha 51, hapa Waziri au Mkurugenzi kwa ridhaa ya Waziri anaweza kutoa kibali cha ukamataji wa wanyamapori. Kwa kutumia kanuni na masharti yote ya sheria na kanuni za uakamataji ndipo anaweza kutoa kibali.
15.Masharti ya jumla kuhusu kibali cha ukamataji (General provisions
Relating to capture permits)
Kifungu cha 52, kinaeleza kibali cha ukamataji kinatakiwa kieleze mahali au sehemu ambayo ukamataji utafanyika. Pia muda wa matumizi ya kibali utaelekezwa na Mkurugenzi.
16.Ukamataji wa wanyama kinyume na sheria (Unlawful capture of an animal)
Sheria imeweka wazi kabisa kuanzia kifungu cha 53 chote, mtu hataruhusiwa kukamata wanyama bila kibali, au kukamata wanyama ambao hawajatajwa kwenye lesseni yake au kukamata wanyama ambao wapo kwenye majedwali tofauti na aliloelekezwa kukamata. Pamoja na adhabu ya kukamata wanyama kinyume na utaratibu na maelekezo ya sheria.
17.Utalii usiohusisha Matumizi ya wanyamapori (Non consumptive wildlife utilization)
Sheria inaelekeza katika kifungu chote cha 54, masharti ya kufanya aina hii ya utalii, hakuna mtu yeyote atakaye ruhusiwa kufanya utalii wa picha au talii mwingine usiohusisha matumizi ya wanyamapori bila kibali au lesseni. Kulingana na sheria ya utalii ikiwemo ya mwaka 2008.
18.Uwindaji wa wanyamapori ambao hawapo kwenye jedwali bila kibali (Hunting of unscheduled animals without permit)
Kifungu chote cha 55, hata kama mnyama uliyemwinda hayupo kwenye jedwali, kwa mujibu wa sheria hii hatakiwi kuwindwa bila kibali au lesseni ya uwindaji iliyotolewa na Waziri au Mkurugenzi wa wanyamapori.
- Kuua watoto na wanyama wa kike wenye mimba hairuhusiwai (Killing of Young animals and female pregnant animal prohibited)
Sheria inakataa kabisa kuanzia kifungu cha 56; uwindaji kwa wanyama watoto ambao bado hawajakua, pia inakataa uwindaji kwa majike ya wanyama wenye mimba au wanaoongozana na watoto wao. Kwa ambaye atakiuka masharti ya sehemu hii ya sheria atabapa adhabu kali na faini au kifungo jelaa.
20.Uwindaji au Ukamataji kwenye ardhi (Hunting or capture on land)
Kipengele hiki cha 57, kianeleza masharti ya kuwinda kwenye maeneo au ardhi ya eneo ambalo lina umiliki wa mtu mwingine, na pia sheria inaelekeza uwindaji kwenye maeneo ya vijiji, masharti ya uwindaji kanuni na mwongozo wa kufuata endapo mtu anataka kuwinda kwenye eneo la ardhi ya kijiji.
- Lesseni Maalumu (Special Licence)
Kifungu cha 58 kinaeleza, Mkurugenzi kwa ridhaa ya waziri anaweza kutoa kibali kwa lesseni maalumu za uwindaji na matumizi ya wanyamapori kwa sababu nzuri ambazo ni kwa maslahi ya umma. Hivyo lesseni hizi hutolewa kwa lengo la kufanya utafiti, maonyesho na mambo ya kitamaduni. Lakini yasihusiane na biashara au mambo binafsi.
22.Ulizi wa Kufuata matakwa ya sheria hii (Security for Complince with this Act)
Kifungu cha 59; Mkurugenzi anahusika na kutoa vibali au lesseni kwa watu anatakiwa awalinde kisheria ili watimize matakwa yao kwa mujibu wa sheria. Hii ni endapo mtu huyo alifuata au anafuata matakwa yote ya sheria hii kwenye uwindaji.
- Lesseni haihamishwi au kumwazimisha mtu mwingine (License not transferable)
Kipengele hiki cha 60, kinaelezea mtu mwenye kibali au lesseni hatakiwi kugawa au kumpa mtu mwingine lesseni yake, sheria inakataa kabisa kutumia lesseni ya mtu mwingine kwenye masuala haya ya matumizi ya wanyamapori
- 24. Mkurugenzi anaweza kuongeza muda wa matumizi ya lesseni (Extension of licenses by the Director)
Kifungu chote cha 62, kinaelezea mtu mwenye mamlaka ya kuongeza muda wa matumizi ya lesseni ni Mkurugenzi wa wanyamapori, na atafanya hivyo kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja tu, na atafanya hivyo mara moja tu na sio kila wakati.
- 25. Mnyama aliyeuwawa kwa ajali au kwa makosa (Animal killed by accident or in error)
Kipengele hiki cha 63, kinaelezea ikiwa mtu ameua mnyama kwa ajali atawajibika kufanya mambo yaliyoelekezwa na sheria hii ikiwemo kutoa mnyama huyo ngozi, pembe, meno na nyara nyingine za serikali kisha atakabidhi kwa watu au mamlaka husika.
- Mkurugenzi anaweza kurekebisha matumizi ya silaha za moto zinazotumika kwenye uwindaji (Director may regulate type of weapons)
Kifungi hiki cha 64, kinaeleza kuna aina nyingi za silaha za moto ambazo hutumika katika masuala ya uwindaji, hivyo kulingana na aina ya mnyama silaha ya aina Fulani hutumika kama sheria ya uwindaji inavyoelekeza.
- Uwindaji usiozingatia sheria, uwindaji usiofaa (Unlawful methods of hunting)
Sehemu ya kifungu cha 65, sheria hii kinaeleza njia ambazo sio sahihi kwenye uwindaji wa wanyamapori. Sheria inakataza kutumia mbwa, sumu, mishale, mashimo au mitego kwenye uwindaji wa wanyamapori.
- Kukataliwa, kusitisha, kubadili au kusimamisha kwa muda matumizi ya lesseni ya uwindaji (Refusal cocellation, variation and suspension oflicense )
Kuna masharti ya utoaji wa kuanzia kifungu cha 66, lesseni au upatikanaji wa lesseni, endapo vigezo vinavyotakiwa kwa ajili ya kupata lesseni havijatimizwa mkurugenzi anaweza kuzuia kutoa lesseni, pia mkurugenzi anaweza kuzuia kubadili au kusimamisha matumizi ya lesseni yoyote endapo atagundua kuna udanganyifu, uongo au kughushi maandishi.
- Kukosa vigezo vya kupewa lesseni (Disqualification from grant of licence)
Katika kifungu cha 67, Endapo mtu ana hatia au ana makosa kwenye matumizi ya maliasili kwenye eneo lolote la hifadhi ya wanyama na misitu, hatapewa lesseni
- Lesseni inaweza kutolewa kwa masharti kulingana na mabadiliko (Licences may be issued or varied subject to conditions)
Kifungu cha 68, ndio kifungu cha mwisho kwa sehemu hii ya saba kinachoelezea, Lesseni inaweza kutolewa na Mkurugenzi kwa kuzingatia sheria hii na masharti yote yanayohusu upatikanaji wa lesseni.
Naomba kwa leo niishie hapa tutaendelea kesho na makala hii, endelea kufuatilia mfululizo wa makala hizi ili upate picha pana unapofanya kazi au shughuli yoyote kwenye sekta hii ufanye kazi kwa ufanisi.
Nakushukuru sana kwa kuwa msomaji na mfuatiliaji wa makala hizi, endelea kujifunza na kufanyia kazi haya ili upate maarifa ya kutosha ufanye kazi yako vizuri kabisa. Pia usiache kutoa maoni, maswali na ushauri wako hapa, tutaufanyia kazi na mambo yataenda vizuri kabisa.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255742092569/ +25568248681
www.mtalaamu.net/wildlifetanzania