Kwa muda wote ambao binadamu wamedumu katika uso wa dunia, tembo pia walikuwepo, lakini sasa tumeingia katika mshtuko mkubwa sana, tunaweza tukawa katika hatua za mwisho kabisa za kuwatowesha milele. Katika maeneo ya savanna ya bara la Afrika ambako ndio viumbe hawa wameishi kwa milenia yote, idadi yao imepungua kwa kiasi kikubwa sana karibu mara tatu ya tembo wote kuanzia mwaka 2007- 2014. Katika misitu ya Afrika ya kati, wamepungua kwa asilimia 66, kati ya mwaka 2008 – 2016. Kila siku tembo wengine 55 huuwawa. Na nyuma ya janga hili kuna kitu kimoja tu ndio hupelekea haya yote; uhitaji wa meno ya tembo.
Mwishowe, serikali zimeamka na kuanza kuchukua hatua, kuzuia wanaoua tembo kwa ajili ya masoko ya meno ya tembo duniani kote, na kutambua kuwa uwindaji halali wa tembo ndio huchochea uhitaji wa mweno ya tembo, na pia uwindaji halali wa tembo ndio unaofunika uwindaji haramu au ujangili wa tembo kutofahamika. China wamechukua hatua kuzuia meno ya tembo na pia kufunga biashara yake ya meno ya tembo. Pia Hon Kong wamepitisha sheria ya kufanya hiyo. Marekani nao wamechukua hatua ya kufunga karibia kila biashara za meno ya tembo kwenye maeneo yao, Umoja wa Ulaya nao wamefuta utaratibu huo wa kufunga biashara hizo haramu ambazo zinachochea mauaji ya tembo.
Licha ya kuwa ni wahisani wa kubwa wa uhifadhi wa tembo katika bara la Afrika, bado Umoja wa Ulaya una bishara nzuri sana ya meno ya tembo iliyoshamiri katika masoko ya ndani. Ndani ya umoja wa Ulaya ni halali kufanya biashara bila zuio lolote, ya vitu vilivyotengenezwa na meno za tembo ambavyoo yamepatikana kabla ya mwaka 1947.
Kwa mara ya kwanza biashara hii imegundulika kuwa inafunika biashara zote haramu zinazoendelea katika umoja huu wa Ulaya. Kumekuwa na uvumi wa taarifa kuwa nchi za Ulaya zinauza na kununua mapambo ya kale ambayo yametengenezwa na meno ya tembo, lakini biashara haramu inajumuisha mapambo hayo yaliyotengenezwa na meno ya tembo ambao wameuwawa katika miaka ya hivi kabirbuni.
Katika kujifunza na kutafiti bidhaa mbali mbali zilizotengenezwa na meno ya tembo, tume ya umoja wa Ulaya ilibaini yafuatayo;
Robo tatu (74.3%) ya meno ya tembo yaliyofanyiwa utafiti yamegundulika kuwa ni mapambo kale yaliyotengezwa na meno ya tembo ambayo yalipatikana kwa njia haramu.
Moja ya tano (19%) kati ya vipande vya meno ya tembo vilivyotafitiwa ilionekana kuwa vimetoka kwa tembo ambao waliishi miaka ya 1990 na 2000 waliuwawa baada ya dunia kupitisha sheria ya kuzuia ujangili.
Hili ndio tatizo la umoja wa Ulaya, kwamba kila nchi ambayo ilichunguzwa na kutafitiwa iligudulika wanajihusisha na biashara hii haramu kwa mwavuli wa kufanya biasharaa halali.
Majaribio ya hivi karibuni ya meno ya tembo yalifanyika baada ya mwaka 2010.
Hii ni wazi kuwa umoja wa Ulaya ulikuwa haujasimamia ipasavyo sheria za meno ya tembo, na biashara haramu za meno ya tembo kufanyika kwa uwazi katika maduka na kwa njia ya mtandao karibu kila sehemu ya nchi hizo. Tume ya Ulaya inapitia tena mazuio ya Umoja wa Ulaya kuhusu biashara ya meno ya tembo kama yanaendana na kile wanachokitaka.
Katika ripoti hii kila kitu kimeelezwa kuhusiana na mwafaka huo na hatua za kuchukua. Kuhakikisha tembo wanahifadhiwa na kulindwa, tume inatakiwa kuhakikisha kuwa mianya yote ya biashara haramu inafungwa na pia bidhaa zote za kale zilizotengenezwa na meno ya tembo zinafungiwa kabisa, pia kuzuia kabisa uagizaji wa meno ya tembo kutoka Ulaya na kufunga kabisa masoko ya ndani ya meno ghafi ya tembo. Kwa kufanya hivyo ndio njia pekee kutunza hadhi Ulaya kama kiongozi katika mapambano haya dhidi ya ujangili wa tembo Afrika.
Ndugu msomaji wa makala hii, hapa nimechambua sehemu ndogo tu ya uchambuzi wa ripoti hii iliyokwenda kwa jina la “EUROPE DEADLY IVORY TRADE” ambayo imesheheni habari za kina kuhusu biashara hii ya meno ya tembo kwa nchi za Umoja wa Ulaya. Hivyo basi ili uchambuzi huu usiwe mrefu sana, nimechambua kwa vipengele vidogo vidogo. Nakushauri baada ya kumaliza kusoma utangulizi huu endelea kusoma makala inayofuata ili kujua zaidi kwa undani.
Naamini utangulizi huu umekupa mwanga na ufahamu kuhusu biashara ya meno ya tembo katika umoja wa Ulaya. Endelea kusoma makala zijazo.
Mchambuzi wa ripoti hii ni;
Hillary Mrosso
+255 683 862 481
www.mtalaamu.net/wildlifetanzania