Habari msomaji wa Wildlife Tanzania, karibu kwenye makala ya leo ambayo tutajifunza kwa pamoja mambo mambo yote tuliyoyachambua ndani ya sehemu hii ya saba. Hii ni sehemu nzuri sana na yenye vipengele vingi vinavyohusu, uwindaji, matumizi ya wanyamapori na utalii wa picha au utalii usiohusisha uwindaji wa wanyamapori. Hivyo makala ya leo nimeiandaa kwa ajili ya samari ya sehemu hii ya saba. Hivyo fuatana name kwa mengi zaidi.
- Uwindaji wa wanyamapori
Hiki ni kipengele ambacho kinahusu uwindaji kwa ujumla, masharti na kanuni za uwindaji kamati za ushauri kuhusu maswala ya uwindaji, majukumu ya Waziri kwenye haya maswala, majukumu ya Mkurugrnzi na matakwa ya sheria ya uwindaji. Ushauri kuhusu mambo ya uwindaji na adhabu ya kifungo au kulipa faini kwa ajili ya kukiuka masharti ya uwindaji na kanuni zake. Ni kipengele kizuri sana kwa kufahamu njia zote za msingi kwenye uwindaji wa wanyamapori.
- Waziri anaweza kuzuia utolewaji wa lesseni na vibali
Sehemu hii ya kipengele hiki inaelezea mamlaka ya waziri kutoa au kuzuia vibali vya aina mbali mbali, kwa wageni na wazawa kwenye sehemu hii yameelezwa vizuri na kwa undani zaidi. Na mashareti yote yahusuyo utolewaji wa lesseni na vibali.
- Hakuna uwindaji bila lesseni
Kipengele hiki kinafafanua na kuelezea masharti na mapendekezo ya sheria ya wanyamapori kwamba uwindaji wowote wa wanyamapori hautafanyika bila kuwa na lesseni au kibali.
- Kubadilika kwa majedwali (amendments of schedules)
Kwenye sheria hii kuna majedwali ambayo yamepewa majina mbali mbali ambayo yana wanyamapori wa aina mbali mbali, sheria hii inatoa mwongozo wa namna ya kufanya kwa mujibu wa sheria. Wanyama kwenye majedwali yote yaliyopo humu yanaweza kubadilishwa na kuwekwa kwenye jedwli jingine. Na mamlaka ya kufanya hivyo anayo Waziri.
- Kuwajeruhi wanyamapori
Hiki ni kipengele kinachoelezea endapo mwindaji amemjeruhi mnyama katika harakati za kumwinda anapaswa kuhakikisha mnyama huyo anamuua na asimwache bila kumuua.
- Masharti ya jumla kuhusu lesseni za wanyama wa kuwindwa
Hapa sheria inaelezea masharti ya uwindaji, lesseni na wanyama wa kuwindwa, hivyo ni sehemu nzuri sana ya kujua mengi kuhusu uwindaji na lesseni sahihi za uwindaji.
- Nyara na uwindaji wa kujikimu (Trophy and Subsistence hunting)
Kipengele hiki kinaelezea mambo ya kisheria kuhusu nyara na matumizi mengine ya uwindaji. Wanyama wa kuwindwa na pia nyara zote ambazo serikali imejichagulia kuwa ndizo nyara zake.
- Access to wildlife by traditional community
Hiki ni kipengele ambacho kinaelekeza na kutoa utaratibu wa jamii kuwa na nafasi ya kuwinda na kutumia wanyamapori kwa mujibu wa sheria.
Naomba kwa leo niishie hapa tutaendelea kesho na makala hii, endelea kufuatilia mfululizo wa makala hizi ili upate picha pana unapofanya kazi au shughuli yoyote kwenye sekta hii ufanye kazi kwa ufanisi.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255742092569/ +25568248681
www.mtalaamu.net/wildlifetanzania