Katika mwendelezo wetu wa kuichambua sheria ya wanyamapori sehemu ya saba tutajifunza mambo yote ya msingi yaliyopo kwenye sheria hii muhimu. Katikia kipengele hiki ambacho kinaelezea masharti na mapendekezo ya jumla kuhusu uwindaji. Hivyo ni vizuri tukawa na uelewa wa kutosha kwenye maswala haya ya sheria. Katika mwendelezo wetu wa uchambuzi tutaanzia kifungu cha 54.
- (1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuwinda, kuua au kmjeruhi mnyama haijalishi mnyama huyo ametajwa kwenye jedwali la sheria hii, bila idhini ya kimaandishi kutoka kwa Mkurugenzi. Hivyo katika sheria hii inasisitizwa kuwa uwindaji au uuaji au kumjeruhi mnyama yoyote hata kama mnayama huyo hayupo kwenye jedwali la sherai hii bila ruhusa ya kimaandishi kutoka Mkurugenzi wa wanyamapori ni kufanya makosa, kwa kuwa sheria hairuhusu.
(2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya sehemu hii ya sheria anafanya kosa ambalo litamgharimu kulipa faini ya gharama zisizopungua mara mbili ya thamani ya mnyama huyo aliyeuwawa, kuwindwa au kujeruhiwa au kifungo jela kisichopungua mwaka mmoja lakini kisizidi miaka mitano au vyote kwa pamoja.
56.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuwinda au kuua mnayama yoyote ambaye ni wa kike na mwenye ujauzito au mimba au ambaye anafuatana na mtoto wake. Kwa hiyo hapa sheria inazuia uwindaji wa wanyama wenye mimba na ambao watakuwa na watoto wadogo, hivyo wakati wa kufanya uwindaji unatakiwa kuwa makini sana na kuchagua mnyama ambaye anafaa kuwinda kwa mujibu wa sheria.
(2) Mtu mwenye lesseni, kibali au mamlaka ya kimandishi ya kufanya uwindaji wa wanyama wa spishi yoyote au mtoto wa spishi hiyo au mnyama wa kike wa spishi hiyo ambaye kwa wakati huo atakuwa ana mimba au anaongozana na mtoto wake, isipokuwa mnyama huyo ameelezwa kwenye kibali au lesseni ya uwindaji kwamaba awindwe au kwenye mamalaka ya kimaadishi kwamba wawindwe, akimwinda au kukamata anafanya kosa ambalo litamgharimu kutoa faini isiyopungua mara mbili ya thamani ya mnyama aliyewindwa au kifungo cha miaka mitatu jela au vyote kwa pamoja.
(3) Mtu yeyote atakaye winda mnyama mtoto au mnyama wa kike ambaye ana mimba kwa wakati huo bila lesseni, kibali au mamalaka ya kimaandishi anafanya kosa ambalo atawajibika kutoa faini isiyopungua thamani ya mnyama aliyemuwinda au kuuwawa au kwenda jela kwa kifungo kisichopungua miaka mitano au vyote kwa pamoja.
Uwindaji au ukamataji wa wanyama
Katika sehemu hii inaeleza masharti ya ukamataji wa wanyama kwenye maeneo mbali mbli ya hifadhi ya wanyamapori. Taratibu za kisheria na adhabu kwa wanaokiuka mashrti ya sehemu hii ya sheria.
- (1) Mtu yeyote hataruhusiwa kufanya shughuli za uwindaji au ukamataji kwenye maeneo yanayomilikiwa kisheria au kihalali kwa ajili ya shughuli hizo, isipokuwa mtu huyo ana lesseni, kibali au mammlaka ya kimaandishi ya kufanya shughuli hiyo kwenye maeneo hayo ambayo imetolewa kwa mujibu wa sheria hii kwa ajili ya kuwinda au kukamata mnyama husika.
(2) Mtu yeyote hatawinda au kukamata wanyama katika eneo la ardhi ya Kijiji bila kuwasilisha nakala ya cheti cha kibali au lesseni kwa Baraza la Kijiji, mamlaka ya jumuiya na Afisa Wanyamapori Wilaya. Hivi ndivyo inavyotakiwa kufanyika endapo mtu anataka kufanya uwindaji au uakamataji wa wanyama kweneye eneo la aridhi ya Kijiji.
(3) Nakala ya cheti na lesseni iliyotajwa hapo juu kwenye kifungu kidogo cha pili inatakiwa kubaki kwa Baraza la Kijiji, mamlaka ya jumuiya na kwa Ofisa Wanyamapoiri Wilaya.
(4) Pale ambapo Mkurugenzi ataona inafaa baada ya kupata idhini ya Waziri kwa jambo ambalo lina manufaa kwa umma kwamba mnyama yoyote kwenye ardhi yoyote anatakiwa kuwindwa au kukamatwa anaweza kumruhusu mtu yeyote kuwinda au kukamata mnyama kwenye eneo husika baada ya kuwasilisha nakala ya cheti kwa mamlaka husika au kwa mmiliki na itaruhusiwa kisheria kwa mtu huyo anayetaka kuwinda au kukamata wanyama kuendelea kufanya hivyo bila hata idhini ya mmiliki wa eneo hilo. Kwa mantiki kwamba mtu aliyeruhusiwa kufanya uwindaji au ukamataji kwenye eneo hilo hataingia ndani ya jengo au makazi ya mwenye ardhi bila idhini ya mwenyeji au mmiliki wa eneo hilo.
(5) Mtu yeyote ambaye-
(a) sio aliyetajwa hapo juu na kupewa kibali cha kukamata au kuwinda wanyama katika ardhi ya mtu binafsi bila idhini ya mmiliki wa eneo;
(b) ikiwa mtu huyo aliyepewa mamlaka ya kukamata au kufanya uwindaji atakiuka masharti ya kifungu kidogo cha (4)
(c ) kuwa mmiliki wa eneo hilo la uwindaji kumzuia mtu mwinginge ambaye ana kibali na ameshatoa nakala ya kuruhusiwa kufanya shughuli hizo kwake na kwa mamlaka husika kwa ajili ya kukamata au kuwinda mnayama.
Kwa kufanya hayo yote ni kosa kwa mujibu wa sheria, na atawajibika kutoa faini isiyopungua mara mbili ya thamani ya mnyama au kwenda jela kwa kifungo cha miezi sita lakini kisizidi miaka miwili au vyote kwa pamoja.
(6) Mapendekezo ya kifungu kidogo cha (4) hayata husisha maeneo ya bustani za wanyama (Zoos), mashamba ya wanyamapori (wildlife farms), vituo vya kulelea wanyamapori walio katika matatizo mbali mbali (game sanctuaries), au maeneo ya kutunzia wanyama waliokosa wazazi (orphanage centre) au sehemu nyingine zinazoendana na hizi.
Lesseni maalumu
Katika kifungu hiki cha sheria ndio kinachotoa kibali kwa shughuli mbali mbali za kitaalamu, kiutafiti na kisayansi kufanyika kwenye maeneo ya hifadhi za wanyama. Kwa mfano kuwafunga wanyama sateliti kola, kudati na utafiti mwingine unaohusisha kupiga picha, hii ndio sehemu ya sheria inayozungumzia hatua na masharti ya lesseni maalumu. Ni lesseni inayotolewa kwa wanafuni na watafiti kwenye kitengo hiki cha wanyamapori. Tunagalie sheria inavyoelekeza hapa.
- –(1) Licha ya masharti na mapendekezo ya sheria hii, itaruhusiwa kwa mujibu wa sheria kwa Mkurugenzi, baada ya kupata idhini kutoka kwa Waziri kwa maandishi na iwe ni kwa maslahi ya umma kwa kulipia au bila kulipia kutoa kibali cha lesseni maalumu kwa mtu yeyote kuelezea na kuamuru kwa mwenye lesseni hiyo kuwinda, kukamata au kupiga picha wanyama walioainishwa au kutajwa kwenye lesseni aliyopewa, kwa kusudi la-
- Utafiti wa kisayansi;
- kuonyesha kwenye makumbusho;
- shughuli za kielimu;
- kitamaduni; au
- chakula wakati wa dharura.
(2) Lesseni maalumu iliyotolewa kwenye kifungu kidogo cha (1) inaweza kutoa mamlaka ya kuwinda, kukamata au kupiga picha mnyama yoyote kwa mantiki kwamba mamlaka ya kufanya hivyo yatalenga maslahi mapana ya umma na pia haitakiuka masharti yoyote ya kamataifa yanayohusu uhifadhi na usimamizi wa wanyamapori na maliasili nyingine ambayo Serikali ya ilitia saini au kukubaliana.
(3) Lesseni maalumu inayotolewa kulingana na kifungu kidogo cha (1) hatatumika kwa sababu za kibiashara au sababu binafsi. Hivyo endapo kutatolewa lesseni maalumu basi kutakuwa na vipaumbele ambavyo vinatakiwa kuwa na maslahi mapana kwa jamii na wala sio mambo ya binafsi au kibiashara.
(4) Waziri atatangaza kwenye Gazeti la Serikali kuhusu kanuni na masharti ya aina, spishi, na idadi ya wanyama ambao wataruhusiwa kuwindwa kukamatwa kwa mujibu wa sehemu hii ya sheria. Hivyo ndivyo utaratibu utakavyokuwa kwa watakaotumia lesseni maalumu kwa mujibu wa sheria hii.
Naamini hadi kufikia hapa utakuwa umepata mwanga mzuri kuhusu vifungu vya sheria tulivyochambua siku ya leo. Hivyo endelea kufuatilia na kujifunza hapa kwenye mtandao wako wa wildlife Tanzania, pia ni muhimu tukawashirikisha na wengine maarifa haya muhimu. Hadi siku na wakati mwengine tukutane hapa.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife conservationist
Simu +255 683 248 681/+255 742 092 569
Email hillarymrosso@rocketmail.com
Blog www.mtaalamu.net/wildlifetanzania