Aridhi ni rasilimali muhumu sana kwa nchi  yoyote, hakuna maendeleo yoyote yanaweza kufikiwa bila kuwa na aridhi nzuri na inayozalisha. Tanzania inabaki kuwa ni nchi yenye eneo kubwa kwa ajili ya matumizi mbali mbali ya aridhi. Maeneo makubwa ya aridhi ya Tanzania yanafaa kwa ajili ya kilimo, ufugaji, na shughuli nyingine za maendeleo na uzalishaji. Katika makala hii nimelenga kutoa muelekeo unaoonekana sehemu nyingi kwenye matumizi na umiliki wa aridhi.

Katika zama hizi matumizi ya aridhi yameongezeka sana na watu wengi wanakimbia kutafuta na kuchukua maeneo yenye rutuba kwa ajili ya kilimo na uzalishaji wa bidhaa mbali mbali. Hii ni kutokana na kuwa na fursa nyingi za uwekezaji na uzalishaji kwenye kilimo, hivyo matumizi ya aridhi yameongezeka na yanazidi kuongezeka kila siku.

Ukilinganisha idadi ya watu kwa kipindi hiki imeongeza sana, hivyo matumizi ya aridhi nayo yataendelea kuongeza zaidi. Kwa sasa nchi ya Tanzania ina watu zaidi ya milioni 50, ambao asilimia zaid ya 80 wanategemea kuendesha maisha yao kwa njia ya kilimo. Hivyo lazima matumizi ya aridhi yatongezeka kwa namna yoyote ile.

Jambo zuri kwa nchi yetu ilisha tenga maeneo mbali mbali kwa ajili ya wanyamapori, na misitu, changamoto ipo kwa wafugaji ambao wamenea kila pembe ya Tanzania. Bado kuna maeneo ambayo yana migogoro, watu wengi hawajayaelewa vizuri kuwa yapo kwa ajili ya nini, pia mfano ni sehemu zenye migogoro ya mara kwa mara.

Ili kuwe na mipango mizuri na kuepuka migogoro ya mara mara inayotokea na iakayotokea hapo baadaye ni vizuri serikali ikaja na mipango mizuri ya muda mrefu ambayo itasaidia kutaua na kuweka mazingira yote salama kabisa. Maeneo yote ya aridhi ya Tanzania yanatakiwa kufanyiwa utafiti ili kuyapanga kulingana na shughuli itakayokuwa inafanyika. Kama ni maeneo ya wakulima yapangwe vizuri nay awe ya kutosha, kama ni maeneo ya mifugo yapangwe vizuri na kama ni maeeo ya hifadhi nayo yapangwe. Pia maneo haya yanatakiwa kusimamiwa na kufanyiwa ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kujua changamoto na mafanikio yake.

Mipango ya aridhi  ni muhimu kwa mahitaji ya sasa na baadaye! Ahsante sana

 Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 862 481/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania