Tanzania imebarikiwa kuwa na eneo kubwa sana la ardhi linalofaa kwa matumizi mbali mbali, kama vile kilimo, ufugaji, uvuvi na maeneo yaliyohifadhiwa kwa ajili ya maisha ya wanyama na utalii. Tanzania imebarikiwa kuwa na maliasili nyingi sana zenye thamani kubwa sana, na kati ya hizi maliasili tulizo nazo ni za kipekee yani hazipatikani sehemu nyingine yoyote isipokuwa Tanzania tu.
Pamoja na kuwa na eneo kubwa lenye kufaa kwa matumizi mengi Tanzania inakabiliwa na migogoro mingi ya ardhi ya muda mrefu, na isiyo isha migogoro hii inayotokea kwa wafugaji, wakulima na watu wengine wenye mamlaka imekua ni nyimbo zinazoimbwa kila siku mpya ya wiki. Utasikia mifugo zaidi ya 400 imekamatwa kweneye eneo la hifadhi ya wanyamapori, au utasikia zaidi ya watu wawili na ng’ombe zaidi ya 40 wameuwawa kutokana na ngombe hizo kula na kuharibu mazao na shamba la wakulima walio karibu na wafugaji hao. Hizi ni kelele ambazo zina mizizi yake tokea ukoloni uingie hapa nchini.
Katika kufuatilia na kudadisi wapi shida inapoanzia ilinibidi kuangalia sheria za ardhi na majarida mbalimbali yaliyoonyesha jambo hili kwa upana wake. Hivyo kukuandikia leo ni matokeo ya uzoefu nilio nao kwenye masuala haya na kujifunza kupitia vyanzo mbalimbali vya taarifa. Nimegundua kwa asilimia kubwa hii migogoro inasababishwa na udhaifu uliopo kwenye sheria za ardhi, kwamba hazijatoa mwongozo unaoeleweka kwa wafugaji na maeneo yao. Najua jinsi sekta nyingine zilivyo na sheria na sera zinazotekelezeka kwenye utendaji wa sekta husiuka. Mfano sekta ya maliasili na utalii ipo wazi kabisa kwa sheria na sera zake na muongozo unaoeleweka kwa kila mtu ili kazi zifanyike kwa ufanisi unaotakiwa.
Tafiti nyingi zinazoangalia chanzo cha migogoro hii ziznonyesha kabisa kwamba inapofika kweneye maeneo maalumu yaliyotengwa kwa makusudi maalumu, unakuta sehemu za malisho hazitiliwi mkazo au hazina ubora unaotakiwa, sambamba na hilo maeneo yaliyopo kwa ajili ya ufugaji hayajitoshelezi kulinganisha na maeneo mengine. Kutokujali na kutokuwa na mpango wa kumaliza migogoro hii bado kunaibuka sheria na amri za kuwataka wananchi na wafugaji walio karibu na hifadhi kupisha au kuhamishwa kwa nguvu kupisha uapanuzi wa hifadhi za wanyamapori na maliasili nyingine. Hivyo huzidi kumege na kulipunguza eneo la malisho ya wafugaji hawa, ambayo hupelekea wafugaji kuwa na maisha ya kuhama hama kutafuta malisho na maji, kuhama hama huku ndio huzua migogoro isiyo na mwisho kati ya wakulima na hata wafugaji wenzao waliowakuta huko waliko hamia.
Sijajua vizuri kwanini hakuna mwongozo na maelekezo mazuri kweneye hii sekta ya ufugaji? Au kwa vile haionekani ikichangia pato la nchi kwa kiwango kikubwa kama sekta nyingine, kama vile sekta ya maliasili na utalii, madini, kilimo nk. Au kwa kuwa hakuna faida ya moja kwa moja kwawafugaji inayopatikana kutokana na uwepo wa maliasili hizi kweneye maeneo yao. Mara nyingi mwekezaji anapokuja katika eneo la kijiji ili kupata ardhi ya kuwekeza huwa inaweza kutishia uyanyasaji kweney aneo la malisho ya mifugo wao.
Ndugu msomaji wa makala hii, kwa hali ilivyo sasa hairdhishi serikali iantakiwa kuingilia na kuweka sheria na sera na mwongozo unaoeleweka kwa wafugaji wote ili wasionewe na watu wanaotaka kuchukua maeneo yao. Kwa jinsi mabadiliko ya tabia nchi yanavyo kuja kwa kasi, lazima tuzibe mapema nyufa zote zinzoweza kusababisha ugomvi na migogoro isiyoisha kwenye jamii yetu, ambayo kwa kiasi kikubwa huchangia kupotea kwa amani katika nchi. Tufanye kazi kwa pamoja ili kupunguza hali hii kwenye nchi yetu.
Makala hii imeandikwa na
Hillary Mrosso
0742092569










