Habari msomaji wa blog ya wildlife Tanzania, naamini unaendele vizuri na majukumu yako ya kila siku. Leo tutatumia makala hii kuwapongeza Wizara ya maliasili na utalii pamoja na Shirika la Hifadhi za wanyamapori Tanzania kwa kazi nzuri na bora sana walioifanya kenye msimu huu wa sikukukuu za Nanenane. Ambayo kwa kanda ya kati yamefanyika Dodoma Kitaifa. Naamini kwa wale waliokwenda au waliokuwa Dodoma watakuwa mashahidi wazuri wa mambo haya ninayoyaelezea. Mimi binafsi nilikuwa Dodoma na nilifarijika sana kuona jinsi TANAPA walivyojipanga kuhakikisha wanatoa nafasi kwa wakazi wa Dodoma kutembelea hifadhi kwa gharama nafuu sana ya Ofa.
Nilibahatika kutembelea mabanda ya Wizara ya maliasili na utalii kule Nanenane Dodoma, nilijionea mwenyewe mambo yalivyokuwa yanaendeshwa kwa weledi na utaratibu. Nilipita kuuliza maswali mbali mbali, kupata ufafanuzi na kujua majukumu mbali mbali ya hifadhi za Taifa, pia sikusita kufika kwenye idara kubwa ya wanyamapori ambapo pamoja na mambo mengine hii ndio idara inayohusika na utalii kwa njia ya matumizi ya maliasili, yaani uwindaji wa kitalii, nilikaa kwenye banda hili kwa muda mrefu ili kupata kufahamu majukumu yao, nilijifunza mengi sana ambayo nitakushirikisha kwenye makala ijayo.
Leo sita andika mambo mengi, ila nikama nilivyoelezea ni kuwapongeza Wizara ya Maliasili na Utalii na watu wote wanaofanya kazi kwenye sekta hii. Nawapongeza sana Shirika la hifadhi za wanyamapori Tanzania- TANAPA kwa kufanya jambo hili kwa wakazi wa Dodoma. Naamini mtafanya hivyo kwa wakazi wa mikoa mingine pia, ili kuinua utamaduni wa kutembelea hifadhi za wanyama na vivutio vingine muhimu. Pia kwa kufanya hivyo watu wengi ambao walikuwa hawajui kama kuna hifadhi za wanyama na vivutio vingine watajua na watakuwa mabalozi wazuri kwa kutangaza utalii wetu wa ndani.
Pia nawapongeza wale waliofanikwa kwenda kutembelea hifadhi za Tarangire na Ruaha, nafikiri na naamini mmejifunza na kufurahia mambo mengi mazuri na mtakuwa mabalozi na walimu wazuri kwa watanzania wengine ambao hawakupata fursa hii ya kutembelea hifadhi. Hongereni sana natamani ofa hizi ziendelee kutolewa mara kwa mara ili kuwahimiza watanzania kutembelea hifadhi za wanyamapori na pia itasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya jamii na hifadhi za wanyamapori. Kwa wale waliopata ofa hii msiishie hapo tu, endelea kutembelea na hifadhi nyingine ambazo bado hujatembelea. Hongereni na asanteni kwa kushirikiana nasi katika kuitangaza na nchi yetu kupitia utalii wa ndani.
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569
www.mtalaamu.net/wildlifetanzania