Habari msomaji wa makala za wildlife Tanzania, karibu kwenye makala nyingine ya leo, ni makala nzuri sana, kwa sababu itakujuza mambo mengi ambayo huyajui kuhusu wanyama na ndege, kwa mujibu wa sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009. Sehemu ya mwisho kabisa mwa sheria hii kuna majedwali yanayotaja wanyama na ndege wengi ambao wengine hatuyajui majina yake. Jana tulijifunza big game wote ambao wapo kwenye sheria hii sehemu ya tatu na jedwali la tatu. Leo tuendelee na jedwali la tatu (Third Schedule). Jana tulijifunza wanyama, lakini kwenye makala ya leo tutajifunza kuhusu ndege. Karibu sana tujifunze pamoja tuwaangalie Game birds wote waliopo kwenye sheria hii, ( ninaposema game birds maana yake ndege wanaoruhusiwa kuwindwa au wakuwindwa, lakini wanawindwa kwa kibali maalumu kabisa.
Katika majina haya yametajwa jina la Kiswahili, kingereza, na jina la kisayansi.
Jina la Kiswahili | Jina la Kingereza | Jina la Kisayansi |
Bata bukini mdogo | Piggmy Goose | Nettapus |
Bata bukini | Egyptian Goose | Alopochen |
Bata bukini- bawa kijani | Spurwing Goose | Plectropterus |
Bata domo – kifundo | Knob-billed Goose | Sarkidiornis |
Bata kichwa chekundu | Northern Pochard | Aythya |
Bata kichwa cheupe | White Faced Whislting Ducks | Dendrocyna |
Bata mdogo | Teals | Anas |
Bata- makoa | Maccoa Duck | Oxyura |
Firiogo koo-njano | Yellow- Throated Sandgrouse | Pterocles |
Firingogo tumbo jekundu | Chestnut- bellied Sandgrouse | Pterocles |
Kanga | Helmeted Guinea Fowl | Numida |
Keren’gende | Pur Fowl | Francollinus |
Kituitui tambo | Harlequail Quail | Cortunix |
Kituitui | Common Quail | Cortunix |
Kololo | Crested Guinea Fowl | Guttera |
Kololo tumbusi | Vulturine Guinea Fowl | Acryllium |
Kotwa | White- Backed Duck | Thalasomis |
Kwale | Francolins | Francollinus |
Ninga | Green Pigeon | Treron |
Njiwa | Pigeons | Columba |
Pungi | Doves | Oena |
Pungi | Doves | Turtur |
Tetere | Doves | Streptopelia |
Hivyo kufikia hapa nikuache na makala hii, ujifunze na kujua ndege waliotajwa kwenye sheria ya wanyamapori, wapo aina na spishi nyingi sana za ndege. Hawa ndege niliowataja hapa ni kwa mujibu wa sheria mama ya wanyamapori ya mwaka 2009. Hivyo nikukaribishe kuendelea kujifunza kupitia makala hizi za wanyamapori.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania