“Humanity can no longer stand by in silence while our wildlife is being used, abused and exploited. It is time we all stand together, to be the voice of the voiceless before it’s too late. Extinction means forever.”
                          ― Paul Oxton

Habari msomaji wa Wildlife Tanzania, karibu kwenye tafakari ya nukuu ya leo ambayo nitaielezea maudhui yaliyopo kwenye nukuu hii. Hii ni nukuu ambayo inamhitaji kila mtu kusimama na kusema hapana kwa ujangili na uharibifu wa mazingira na makazi ya wanyamapori. Kwa jinsi hali ilivyo kwenye maliasili zetu za misitu na wanyamapori tunahitaji kuwajibika kwa kiasi kikubwa ili kuzuia kuendelea kuharibika kwa makazi ya viumbe hai.

Mambo mabaya yanayotokea kwenye hifadhi zetu, kama vile ujngili, uchomaji wa moto bila mpangilio, ukataji wa miti hovyo yote haya yamesababishwa na binadamu. Kwa kiasi kikubwa binadamu tumesababisha mambo kuwa magumu, sio kwetu wenyewe tu bali hata kwa viumbe vingine. Kuna watu wanatumia rasilimali hizi kwa ubinafsi, uroho na tamaa, bila hata kuangalia madhara yatakaotokea kwa matendo yao. Mfano watu kulima kwenye vyanzo vya maji, kuharibu maeneo oevu, kumwaga uchafu na maji yenye sumu kwenye makazi muhimu ya viumbe hai na wanyamapori.

Matumizi mabaya, na kutowajibika kwenye usimamizi wa maliasili zetu muhimu. Tumewaona watu wana haribu mazingira tumewaacha, tumeona watu wanaua viumbe hai bila kufuata sharia tumenyamaza, tumeona watu wanafanya ujangili tumenyamaza kimnya na kuona uharibifu mkubwa kwenye maliasili zetu.

Paul Exton kwenye nukuu hii anasema huu ni wakati wetu wa kuamka na kuacha kukaa kimnya kwenye uhifadhi wa wanyamapori, tunatakiwa kusimama pamoja kuzuia, kuongea, kupinga, na kukataa kabisa vitendo vya kijangili kwenye maliasili zetu. Tukiacha maliasili hizi zikapotea na kutoweka hazitarudi tena, tunawajibu huu mkubwa sasa kama watu ambao tumezungukwa na maliasili hizi za thamani. Tuamke na kupambana na vitendo viovu vya ujangili. Tushirikiane na wenzetu na kutoa taarifa za wanaofanya matendo ya ujangili kwenye jamii yetu.

Huu ni wakati wa kutoa sauti zetu, kupambana na ujangali na kuwa sehemu ya watu waliofanya mazingira yetu na mazingira ya viumbe hai kuendelea kuwa salama kwa vizazi vingi vijavyo.

Ahsante sana

 Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 862 481/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania