Hivi tulivyo leo ni matokeo ya maisha ambayo tumechagua kuyaishi hapa duniani, maneno yetu na juhudi zetu ni kwasabu ya uwepo wa watu wengine na juhudi za watu wengine ambao walishatutangulia au wapo hai na tumewaweka mbele yetu kama kiyoo kwenye juhudi na nidhamu tunazojijingea kila siku. Tunayoaandika na kuyaongea siyo kwamba ni mapya, tunayoyafanya sio kwamba ni mapya, ni michango ya watu wengine na mawazo ya watu wengine waliofanya na kutoa kwenye jamii na kwenye maisha ya watu. Hivyo hakuna ambaye ni wa kipekee sana hapa duniani, ila kila mtu anafanya mambo ambayo yalishafanywa na watu wengine na sisi tunayafanya hayo hayo kwa namna ya upekee tuliopewa na Mungu. Na kutumia njia mbali mbali kuwashirikisha na kuwahamasiha wenzetu kwa vipaji vyetu.
Yote yanayofanywa na kuonekana yana mchango fulani kwenye jamii na maisha ya watu ni kwasabubu ya karama ya Mungu na kwa kuwa Mungu ametupa nafasi ya kuishi hapa duniani na nafasi ya kutoa kile alichokiweka ndani yetu kwa ajili ya kuboresha maisha yetu na ya watu wengine. Hivyo kwa juhudi, ufanisi, kazi nzuri na namna yoyote ile imetokea tumefanya mambo makubwa na watu wakaona kustawi na kubarikiwa kupitia kazi zetu mwenye kusifiwa na kuheshimiwa kwenye kila hatua ya mafanikio yetu ni MUNGU pekee. Kwake yeye hakuna mwenye akili na hakuna mjanja. Kila kitu kipo kwa sababu yake mwenyewe na kwasababu Yeye amependezwa na kuwepo kwetu basi tuishi na kufanya kila kitu kinachompendeza.
Tangu nianze kuandika kwenye blog yangu ni miezi sita, nimekuwa nikiandika makala kila siku, na kuwashirikisha watu wengine mambo mbali mbali yahusuyo wanyamapori, mazingira, uhifadhi na utalii. Kwa kuwa nimepata neema hii mbele za Mungu, basi nimeamua kuwa mwandishi kwa njia hii.Pia namshukuru mwandishi mwenzangu Sadick Kashushu kwa makala zake nzuri ambazo zilikuwa zinachapishwa kwenye mtandao huu.
Nawashukuru wasomaji wote wa mtandao wa Wildlife Tanzania, kwa kusoma kazi zangu kwa kipindi chote, nawashukuru sana maana kama msingesoma nisingekua na nguvu na hamasa ya kuandika makala kila siku, hivyo ninyi ni wa muhimu sana kwangu, na pia ninyi ni wa muhimu sana kwenye kujenga utamaduni mzuri kwa watanzania kuhusu maliasili na utalii, naamini kupitia maarifa haya yatakusaidia si wewe tu bali na watu wengine. Nawashukuru walio commets, nawashukuru waliosoma lakini hawakukoment, nawashukuru walio like nawashukuru zaidi walio share makala zangu kwa watu wengine. Pia nawashukuru walionishauri na kunitia moyo, natambua mchango na mawazo, tupo pamoja. Ninyi ni watu muhimu sana kwenye uhifadhi wa maliasili zetu hapa Tanzania.
Nawaahidi mambo mazuri na makubwa kwa mwaka 2018, tuendelee kuwa pamoja kwa kujifunza mambo haya muhimu kwa maliasili zetu. Nawatakiwa kheri na baraka za mwaka mpya 2018. Endelea kufuatilia na kujifunza kupitia mtandao wetu wa www.mtalaam.net/wildlifetanzania na kwa mawasiliano ni 0683862481. Asante sana.
Hillary Mrosso.