Habari rafiki, karibu katika makala yetu ya leo ambayo tunangalia mambo kadha wa kadha ambayo yatatutafikarisha ili tuweze kuchukua hatua stahiki kwenye ukuzaji wa utalii wa ndani. Katika kutafakaria sababu za watu wengi kutotembelea hifadhi za wanyamapori na vivutio vingine, wengi wamekuwa wakisema kuwa hawana pesa za kutembelea hifadhi na wengine hawana kabisa utamaduni wa kufanya hivyo. Jambo hili limenifikirisha na kunipa kuyaangalia maisha na mitazamo ya watu kwenye maisha. Hapa ndipo nikaja na kutambua kuwa suala la kwenda hifadhini ni suala la kifikra kwanza.

Ukichunguza maisha ya watu wengi hupenda kusafiri sana hasa kipindi cha sikukuu, na wengi huenda vijijini kwao wengine huenda kukutana na  wazazi au walezi wao mikoani na hujipanga kwa muda mrefu kwa ajili ya jamabo hili. Kwa mfano kwa hapa Tanzania tuna kabila la Wachaga ambao wana utaratibu wa kwenda kwao kila Krismasi na sikukuu nyingine, hivyo hata kama wapo mkoa gani hufanya safari ya kurudi kwao kwa sababu mbali mbali, hasa siku za nyuma walitumia sana utaratibu huu. Pia kuna makabila mengine hufanya hivyo, nimechukulia Wachaga kama mfano tu ulio hai, lakini haimaanishi wengeine hawana utaratibu huo. na kuwa na utaratibu wa kutembelea kwenu sio jamba bay ahata kidogo.

Hivyo kwa kusafiri kwa sababu mbali mbali hutumia fedha nyingi zaidi ya hata ambazo wangetumia kwenye utalii wa ndani. Sikatai kwamba kutembelea hifadhi au maeneo yaliyohifadhiwa kuna gharama ambazo utalazimika kuingia, na inategemea unatembelea vivutio gani na sehemu gani, kwa mfano upo mkoani Mbeya na unataka kutembelea Hifdha ya Taifa ya Kilimanjaro moja kwa moja gharama zitakua kubwa sana kuliko ungetembelea hfadhi ya Taifa ya Katavi.

Ndio maana nimeandika makala hii kwako kukupa umuhimu wa kutembelea maeneo yaliyo hifahiwa au vivutio vingine tulivyo navyo. Lengo langu ni kukujengea fikra za kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio tulivyo navyo. Kwa hiyo ukiwa na fikra hizo kwenye akili yako utajipanga na kuhakikisha ikifikia kipindi fulani nitakwenda kutembelea kivutio fulani, hivyo utajiandaa kwa fedha na maandalizi mengine, hata kama maandalizi yatachukua mwaka mzima ni bora kuliko kutokuwa na utaratibu wa kufanya hivyo. Kama tunaweza kusafiri kila Krismasi kwenda sehemu mbali mbali basi tunaweza pia kusafiri kwenda kutembelea vivutio mbali mbali tulivyo navyo.

Ahsante sana rafiki kwa kusoma makala hii, tujipange kiakili na kifedha kutembelea vivutio vyetu, inawezekana kabisa.

Hillary Mrosso

0742092569/0683248681

hillarymrosso@rocketmail.com