Habari Rafiki yangu mpendwa, karibu kwenye makala ya leo ambayo nitaangazia baadhi ya mambo muhimu sana ambayo kila mtu anapaswa kuyafahamu ili ajue nini cha kufanya na maisha yake. Kujitambua inahusisha ufahamu wa kuwa majukumu yote yanayohusu maisha yako ya sasa na baadaye unayakabili mwenyewe bila kufikiria kuwa kutakuwa na msaada au kutegemea msaada wa watu wengine.

Kwenye maisha kuna majukumu ya msingi ambayo yanamuhusu kila mmoja wetu, na pia kuna majukumu yanayoihusu serikali kufanya kwenye jamii husika. Nimeandika haya yote kwa sababu ya hali ya mambo ilivyo kwenye jamii nyingi ambazo zipo pembezoni mwa hifadhi za wanyamapori na jamii nyingi ambazo zipo maeneo mengine ya nchi.

Jamii zinazoishi kando ya maeneo yaliyohifadhiwa ya wanyamapori na misitu wanakabiliwa na changamoto nyingi lakini pia wanapata manufaa ya uwepo wa rasilimali hizi muhimu za wanyama na mimea. Hivyo licha ya kuwa wanapata faida ya uwepo wa wanyamapori pia wanapata changamoto za aina nyingi kama vile uharibifu wa mazao  na mifugo yao na wanyamapori.

SOMA: Tafakari Yangu Na Changamoto Za Uhifadhi Wa Maliasilii

Pia wakati mwingine wanyamapori hawa wamekuwa hatari kwa maisha ya jamii za watu hawa. Mfano wanyamapori kama tembo na simba wameripotiwa sehemu nyingi kusababisha madhara hata vifo kwa watu. Hivyo kuishi na wanyamapori ni changamoto kubwa ambayo inawakabili jamii hizi.

Pamoja na kuwa kuna manufaa yanayotolewa kwa jamii hizi, napia kuna ahadi ambazo mashirika na hata serikali imeahidi kuisaidia jamii hizi. Maeneo mengi yamesaidiwa sana ana miradi na pia serikali kwenye sekta za elimu, afya, maji, na miundombinu ya barabara. Hivyo hiyo ndio misaada iliyotolewa na wadau wa uhifadhi.

SOMA: LEO KATIKA UHIFADHI Vyenye Thamani Hulindwa Kwa Gharama Kubwa

Licha ya misaada hiyo kutolewa na miradi hii changamoto ya maisha imezidi kuwa kubwa. Na mapaka sasa hakuna njia ya uhakika ya kuzuia changamoto hizo, na jamii imekuwa ikivumilia wanyama hawa kwenye maeneo yao.

Ndugu yangu ninachotaka kusema ni kwamba changamoto hazitaisha kwenye maisha na kama utaendelea kuishi maeneo hayo changamoo za wanyamapori zitakuwa ni hizo wakati wote. Na manufa yanayotolewa hayatakuja kumaliza matatizo yako yote, hivyo jua kuwa maisha yako ni muhimu na uchukue hatua stahiki ili kuamuaa licha ya changamoto hizo, bado utaendelea kuishi maisha yako na pia utakuwa na njia nyingine za kujipatia kipato.

Kamwe usitegemee misaada ya serikali kuwa itakuvusha na kutatua kabisa changamoto za maisha yako yote. Inaweza kukusaidia kwa kiasi fulani lakini nakwambia mzigo mkubwa na kazi kubwa inabakia kwako. Hivyo pambana kuhakikisha unafanikiwa kwenye maisha yako licha ya changamoto hizo zote.

Hillary Mrosso

+255 683 862 481

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtalaamu.net/wildlifetanzania