Habari msomaji wa wildlife Tanzania, karibu kwenye mfululizo wa makala nyingine ya leo ambao tunaichambua sheria ya uhifadhi wa wanyamapori ya mwaka 2009. Leo tuaichambua sehemu ya Saba. Ni sehemu nzuri sana ya sheria hii kwani inaelezea matumizi ya wanyamapori kama vile uwindaji na matumizi yasiyo ya uwindaji. Katika uchambuzi wa sheria hii wamegawa vipengele viwili ambavyo kila kimoja tutakichambua ili tuelewe yaliyomo kwenye kipengele husika kwa mujibu wa sheria hii ya wanyamapori. Matumizi hayo ya wanyamapori ni matumizi ya Uwindaji na matumizi yasiyo ya uwindaji kama vile utalii wa picha na kuangalia wanyama bila kuchukua sehemu yoyote ya mnyama huyo. Katika muendelezo wa sheria hii tutaendelea na kifungu cha 38.
Kwa kuwa kifungu hiki kinaanza na matumizi ya wanyamapori au uwindaji wa wanyamapori, sheria hii inataka kama ilivyoainishwa kwenye sheria hii kwamba
38.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji ambayo itakuwa ni chombo cha kumshauri Waziri.
(2) Waziri atamteua Mwenyekiti wa Kamati ya Usahauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji ambaye atakuwa ni mtu mwenye uelewa wa kutosha na uzoefu kwenye mambo ya uhifadhi wa wanyamapori. Kwa hiyo hapa mwenyekiti wa kamati ya ugawaji wa vitalu ambaye atamshuri waziri kwenye mambo yote ya uwindaji anatakiwa kuwa na uelewa na uzoefu kuhusu wanyamapori na uhifadhi wao.
(3) Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji itatakiwa kuwa na wajumbe wafuatao walioteuliwa na Waziri-
(a) Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania;
(b) Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania;
(c) mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
(d) Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori;
(e) watu wowote watano watakaoteuliwa na Waziri; na
(f) Mkurugenzi wa Wanyamapori ambaye atakuwa Katibu wa Kamati.
(4) Katika uteuzi wa mtu ambaye sawa sawa na aya (e ) ya kifungu kidogo cha (3) Waziri anatakiwa kuzingatia uhitaji wa usawa kijinsia, uelewa na uzoefu katika masuala ya usimamizi wa biashara, masuala ya uhifadhi wa mazingira yanayoendana na uwezeshwaji kiuchumi.
(5) Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji itafanya-
(a) kupokea na kujadili hali ya uwindaji na ugawaji wa vibali vya uwindaji na vitalu;
(b) kurejea au kupitia na kutoa ushauri kwenye viwango vyovyote, maelekezo na kanuni kuhusiana na kutolewa kwa vitalu vya uwindaji na jambo lolote linalohusiana na vitalu vya uwindaji;
© Kumshauri Waziri kwenye mambo yanayohusiana na maombi, masharti, utolewaji na vigezo vya ugawaji wa vitalu vya uwindaji;
€ kufanya shughuli nyingine zinazohusiana na utoaji wa vitalu vya uwindaji kama Waziri atakavyo elekeza.
(6) Waziri atagawa kitalu cha uwindaji kwa mwombaji baada ya kupata ushauri wa Kamati.
(7) Licha ya mapendekezo yaliyotolewa kwenye kifungu kidogo cha (6), mtu hataruhusiwa kwa namna yoyote ile,kugawiwa zaidi ya vitalu vitano vya uwindaji ambavyo vitakuwa na vya viwango na ngazi au vigezo tofauti.
(8) Muda wa kumiliki haki ya kitalu chochote cha uwindaji unatakuwa ni miaka mitano na baada yah apo kufanyiwa maboresho, kwa minajili kwamba hakuna maboresho mengine yalishafanywa isipokuwa mwombaji amefikia kiwango cha chini kama ilivyoainishwa kwenye kanuni.
(9) kiasi cha chini kinachozungumziwa katika kifungu kidogo cha (7) itatakiwa kuwa na ukadiraiji wa matumizi na tathimini ya kiutendaji ya mwaka na utendaji wa kitalu cha uwindaji ambayo ilifanywa kwa mwaka wa tatu wa muhula wa uwindaji.
(10) Masuala yanahusiana na aina, ukubwa, na ubora wa vitalu vya uwindaji itaelezwa kwenye kanuni.
(11) Waziri atahakikisha kwamba hali yoyote au mfumo unaotumika katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji ni wa wazi na unaendana na kanuni nzuri za uongozi.
Ndugu msomaji wa makala hizi za uchambuzi wa sheria ya wanyamapori kufikia hapa nadhani utakuwa umepata uelewa wa utaratibu wauwindaji kwenye sekta ya wanyamapori Tanzania. Kina mengi ya kuelezea hapa ila leo tutafakari hayo, Kesho tutaendelea na kifungu cha 12.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania