Habari msomaji wa makala hizi za wanyamapori, karibu tuendelee na uchambuzi wa ripoti yetu iliyokuwa inahusu kushamiri kwa biashara haramu ya meno ya tembo barani Ulaya ilivyochangia kuongezeka kwa vitendo vya kijangili kwa sababu biashari hiyo ilikuwa ni mwavuli wa biashara nyngine haramu kufanyika bila kugundulika kwa urahisi. Jina la ripoti tunayoichambua ni “EUROPE DEADLY IVORY TRADE”
Tuendelelee na uchambuzi huu, na sehemu hii tutaelezea njia bora kabiasa ya kisasa ambayo inatumika kugundua umri wa meno ya tembo kwa kutumia kifaa kinachoitwa RADIOCARBON TESTING.
Kwa siku za hivi karibuni umoja wa Ulaya ulisema kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa vifaa na bidhaa za mapambo ya kale yaliyotengenezwa na meno ya tembo kuwa yanachochea biashara haramu ya meno ya tembo na hata ujangili. Ili kupatikane ushaidi kwamba nchi za umoja wa Ulaya zinazojihusisha na biashara ya visanamu na mapambo ya vitu vya kale ambavyo vimetengenezwa na meno ya tembo, kuwa biashara hiyo ni mwavuli wa biashara haramu ya meno ya tembo, na pia hakuana uhakika kuwa meno ya tembo yaliyotengeneza mapambo hayo kuwa ni ya zamani au ya kabla ya miaka 1947.
Ili ukweli ujulikane, hatua za makusudi zilichukuliwa ambapo ilipendekezwa kuwa utafiti wa kisayansi ufanyike ili kubaini ukweli wa mambo, na hapo ndipo vipande 109 vya meno ya tembo kutoka katika nchi mbali mbali za umoja wa Ulaya vilinunuliwa, na shirika la kitafiti la Elephant Action League walitoa msaada mkubwa kufanikisha upatikanaji wa vipande hivyo kwa ajili ya utafiti.
Bidhaa zote zilizonunuliwa kwa ajili ya utafiti zilichaguliwa kwa vigezo vya kuangali vyeti vya biashara hiyo, miaka, bei na sehemu zilipotoka bidhaa hizo kuhakikisha kila bidhaa muhimu zinazohitajika kwa utafiti zinakuwepo. Haijalishi bidhaa hizo zimetangazwa kutengenezewa na maeno ya tembo yaliyopatikana kabla ya 1947 au la. Baada ya hapo zilichukuliwa kwa ajili ya uchunguzi katika maabara ya radiocarbon iliyopo katika chuo kikuuu cha Oxford nchini uingereza kwa ajili ya kufanyiwa utafiti.
Matokeo ya utafiti huo ulionyesha bila shaka yoyote kuwa bidhaa zote za mapambo zilitengenezwa na meno ya tembo ambayo yaliuzwa katika nchi za Ulaya yalipatikana kwa njia haramu na sio kweli kuwa meno hayo ya tembo yalipatikana kabla ya mwaka 1947 kama wanavyosema wanaojihusisha na biashara hiyo.
Na pia utafiti ulibaini kuwa bidhaa za meno ya tembo zilizokuwa zinauzwa kwenye masoko na kwenye maduka mbali mbali katika nchi za umoja wa Ulaya, ni tembo ambao wameuwawa miaka ya hivi karibuni na hakuna cheti chochote cha uhalali wa kufanya biashara hiyo kwa wafanyabiashara hii ya meno ya tembo, wenyewe walikuwa wanasema tu kwa mdomo kuwa bidhaa zao au meno hayo ya tembo yemepatikana kabla ya mwaka 1947.
Hivyo kwa utafiti huu ulionyesha kwenye baadhi ya nchi zilizochunguzwa kuwa bidhaa zote zilizokuwa zinauzwa zilikuwa ni bidhaa haramu, nchi hizo ni Bulgaria, Uhispania, Italia, Ufaransa na Uholanzi, tafiti zimebainisha kuwa bidhaa zilizotengenezwa na meno ya tembo zilikuwa sio halali kabisa, kwasababu zilionyesha tembo walioishi baada ya mwaka 1947.
Teknolojia hii mesaidia sana kumaliza ubiashi ambao ulikuwepo, na pia umesaidia sana kwa nchi wanachama wa umoja wa Ulaya kuchukua hatua za haraka kusitisha biashara za meno ya tembo kwenye masoko ya ndani.
Usiache kufuatilia uchambuzi unaofuata kujua matokeo ya utafiti kwa kutumia Radiocarbon. Hii ni sehemu ndogo ya uchambuzi wa ripoti hii, endelea kufuatilia na kujifunza ili kujua na kuchukua hatua.
Asante sana!
Mchambuzi wa ripoti hii ni;
Hillary Mrosso
+255 683 862 481
www.mtalaamu.net/wildlifetanzania