oooo

internet

Faru ni mnyama wa pili kwa ukubwa duniani baada ya tembo kwa wanyama waishio nchi kavu. Kuna jamii tano (5) za faru duniani kote. Kati hizo jamii 5, mbili hupatikana barani Afrika na tatu hupatikana bara la Asia. Jamii za faru wanaopatikana barani Afrika ni Faru Weusi na Faru Weupe na wote hawa wakiwa na pembe mbili kichwani. Jamii za faru wanaopatikana barani Asia ni Faru Javan, Faru Indian na Faru Sumatran. Faru Javan na Faru Indian ni jamii ya faru wenye pembe moja tu kuchwani isipokuwa faru Sumatran pekee tu undo mwenye pembe mbili kama walivo faru wanaopatikana bara la Afrika.

SIFA ZA FARU

  1. Ni wanyama walao majani
  2. Wana miili mikubwa nah ii kufanya kuwa wapili kwa ukubwa kwa wanyama waishio nchikavu baada ya tembo
  3. Ni wanyama wenye uwezo wakuona vizuri mchana tu
  4. Tofauti na jamii zingine, faru wapatikanao bara la Afrika hawana meno sehemu ya mbele ya midomo yao
  5. Wana pembe ambazo huwasaidia kupambana na adui zao wakati wa hatari
  6. Ni mnyama anaeishi katika mipaka yake alojiwekea (wanaishi kwa kujitenga)

 

Kwa ufahari,thamani na heshima tuwazungumzie faru wapatikanao bara letu la Afrika ambao ni faru mweupe na faru mweusi

                                                    FARU MWEUPE NA FARU MWEUSI

Ifahamike kuwa majina haya hayatokani na rangi za ngozi zao. Kuna baadhi ya sifa tofauti walizonazo wanyama hawa hivo kupelekea mmoja kuitwa faru mweupe na mwingine faru mweusi.

Sababu kubwa iliofanya jamii moja kuitwa faru weupe na nyingine kuitwa faru weusi ni kutokana na maumbile ya midomo yao. Na hasa hii ilitokana na lafudhi ya baadhi ya jamii za watu wa Afrika walipokuwa wakitamka neno  “wyd”  au “whyde” wakimaanisha “wide” yaani pana. Hii ilitafsiriwa vibaya nakuchukuliwa kama neon “white” (nyeupe). Neno wyd lilikuwa likitumika kwa faru mweupe kwasababu mdomo wake ni moana na butu nah ii hasa ndo tofauti kubwa kati ya faru mweupe na faru mweusi. Neno faru mweusi lilikuja tu ili kutofautisha jamii hizi mbili. Mdomo wa faru mweusi umechongoka tofauti na ulivo wa faru mweupe.

Hii pia hupelekea faru mweusi kuwa wanakula majani machanga ya juu hasa kwenye vichaka vidigi vidogo na faru mweupe kutokana na umbo la mdomo wake hula majani ya chini kama walavyo ng’ombe.

Tofauti nyingine kati ya faru mweupe na faru mweusi ni kama inavyooneshwa kwenye jeduwali hapa chini.

SIFA FARU MWEUPE FARU MWEUSI
Kimo Futi 5-6 Futi 4.5-5.5
Urefu Futi 12-15 Futi 10-12
Uzito Kg 1600-kg2400 Kg1600-kg1800
Kichwa Kikubwa zaid Kidogo

 

Pia faru mweupe anapoongozana na mwanae humtanguliza mbele lakini faru mweusi hutangulia yeye kasha mwanae hufata nyuma.

  MAZINGIRA

Faru wanauwezo wakuishi katika mazingira tofauti hususan maeneo ya misitu yenye mvua na aridhi yenye uwezo wakutunza maji kwa muda fulani. Hivo hufanya wanyama hawa kupendekea sana maeneo yenye maji yakutosha.

CHAKULA

Faru ni mnyama miongoni mwa jamii ya wanyama wanaokula majani na mara chache mahome ya miti.

                                              KUZALIANA

Dume na jike maranyingi hupigana sana wakati wanapotaka kujamiiana na wakati mwingine hupelekea mpaka kuumizana na kutoana madonda kutokana na pembe zao. Mara tu baada ya kujamiiana kila mmoja huenda kivyake na kuishi katika mipaka au eneolake alojiwekea chini ya himaya yake.

Jike hubeba mimba takribani miezi 14-18 na huzaa motto mmoja tu. Mtoto huanza kula ,ajani kwa muda wa wiki moja tu baada ya kuzaliwa. Mtoto huwa chini ya uangalizi mkali wa mama kwa muda wa mwaka mzima. Kati ya umri a miaka 2-4 ndipo mtoto na mama hutengana . Watoto wa kike huendelea kubaki na mama zao wakati watoto wakiume huondoka na kwenda kuanzisha makazi mapya maeneo mengine.

Kipindi mama analea mtoto uwa na hasira sana na kamwe uwa hakubali kuruhusu dume kumsogelea karibu. Hii hupelekea tofauti ya myaka 5 kati ya mtoto mmoja na mwingine. Ivyo kupelekea madume wengine kuuwa watoto ili kumfnya mama awe tayari kubeba mimba nakuzaa tena.

UHIFADHI WA FARU

  • Faru ni miongoni mwa wanyama waliohatarini kutoweka duniani kutokana na vitendo vya ujangili. Takwimu za sasa zinaonesha kupungua kwa kiasi kikubwa cha idadi ya faru ukilinganisha na hapo zamani
  • Mpaka kipindi cha mwanzoni mwa nusu ya karne ya 20 idadi ya faru hususan faru weusi barani Afrika ilipungua kwa makadirio ya faru 70,000 mwanzoni mwa myaka ya 1960 na kurekodiwa kwa kiasi kidogo cha faru 2,410 mwaka 1995.
  • Hebu angalia jumla ya faru barani Afrika kwasasa inakadiriwa kuwa ni faru 25626, ambapo

Faru weusi ni 5,042-5,455

              Faru weupe ni 19,682-21,077

  • Jitihada kubwa zina hitajika ili kunusuru kutoweka kwa wanyama hawa.

                                            CHANGAMOTO KUBWA

  • Tatizo kubwa linalopelekea idadi ya faru kupungua ni ujangili. Hii ni kutokana na thamani kubwa ya pembe ya faru na hasa kwa ajili ya biashara kwa nchi zilizo endelea.
  • Pembe ya faru imekuwa ikitumika kama dawa za asili kwenye baadhi ya nchi lakini pia kama mapambo ya ndani.
  • Hii hufanya wanyama hawa kuwindwa na kuuliwa kwa kiasi kikubwa sana na hata baadhi ya malighafi zao kuibiwa maeneo ya makumbusho na sehemu za uhifadhi.
  • Changamoto nyingine ni biashara haramu ya wanyamapori na malighafi zao.

                       NINI KIFANYIKE KUWANUSURU FARU HUSUSA TANZANIA

  • Kukomesha kabisa mahitaji ya pembe za faru.
  • Kuwepo/kutungwa kwa sheria kali zitakazo pambana na biashara haramu ya pembe za faru nchini.
  • Kuepuka kuhusisha siasa katika suala zima la uhifadhi wanyama pori
  • Kubuni miradi mbali mbali ya maendeleo hasa kwa jamii zinazoishi pembezoni mwa hifadhi za taifa na mapori ya akiba. Kwakufanya hivi jamii hizi watakuwa ni mabalozi wazuri katika kuwafichua na kutoa taarifa kuhusu majangili sehemu husika.
  • Kutumia zana za kisasa za kufuatilia maisha ya faru masaa 24 awapo hifadhini kama wanavyofanya wenzetu Afrika Kusini.

 

                                                         HITIMISHO

  • Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo bado tunajivunia kuwa na faru japo ni wachache sana. Kuna baadhi ya nchi faru wametoweka kabisa na utazunguza nchi nzima hutoona faru hata mmoja. Serikali inatumia gharama kubwa sana kuhakikisha faru wetu wanatunzwa na kuzaliana angalau idadi ya faru iongezeke kutoka hapa tulipo sasa
  • Hebu fikiri ndugu mtanzania, faru ili azae tena ni mpaka mtoto afikishe miaka 5 na tena huzaa mtoto mmoja tu. Unadhani lini idadi ya faru itaongezeka kama ilivyokuwa hapo zamani?
  • Ila kwa tama za wachache na uzembe wa watendaji wanaohusika na uhifadhi na utunzaji wa rasilimali zetu za wanyamapori waliopo maliasili faru wetu wanaanza kupotea tena.

                                                             “NAKUKUMBUKA FARU JOHN”

Ukitaka kujua mengi kuhusu wanyamapori wasiliana na mimi kupitia

Simu-0714116963/0765057969 au 0785813286

Email-swideeq.so@gmail.com

                      Mhifadhi wanyamapori toka Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine

Remember………………..”I’M THE METALLIC LEGEND”