Habari msomaji wa mtandao wa Wildlife tanzania, karibu kwenye makala ya leo ambayo tunaangalia na kujifuna tunapotembelea vivutio na hifadhi za wanyama. Ninaamini kabisa kwamba njia nzuri kabisa ya kujua kitu ni kwenda kwenye eneo la tukio na kuona kinachofanyika, huwezi kuelewa kitu vizuri na kukieleea kwa wengine kama haukuona kitu hicho kinavyofanyika. Na hii ni dhana ambayo nataka tuitumie kwenye kukuza utalii wetu wa ndani na nje, endapo tutatumia kanuni hii muhimu tutakuwa na mabaloi wengi watakao kuwa wanaongea mazuri na kuitangaza Tanzania kimataifa kwenye masuala ya utalii na vivutio vyake.
Kuna jambo ambalo tunaweza kulifanya, jambo hili ni kutengeneza mabalozi wengi watakaoitangaza Tanzania kwenye masuala ya vivutio vyake na utamaduni wake. Kwa misingi ambayo tunatakiwa kuiweka ni kwa kuanza na sisi wenyewe. Tunatakiwa sisi ndio tuwe msitari wa mbele kuzielewa maliasili zetu vizuri zaidi, hivyio tunapaswa kuwa na utamaduni wa kutembelea hifadhi za wanyama, sehemu za kihistoria, fukwe za bahari na sehemu nyingine za utamaduni wetu ambao tunauenzi na kuutunza kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Nakumbuka kipindi nikiwa mwanafunzi, nilifurahi sana kutembelea makumbusho ya taifa na kujionea vivutio mbali mbali vya kihistoria ambavyo nilikuwa sijui kama vipo Tanzania, tena niliona kazi nyingi nzuri za mikono iliyofanywa na mababu zetu huko zamani, jambo hili lilinifurahisha sana na kunitafakarisha, pia niliona vifaa na zana za kivita, zilizotumika kipindi cha ukoloni, kwa kweli jambo hili lilinipa hisia nzuri na za kujisemea mwnyewe kama serikali isingekuwa na hekima ya kuhifadhi vitu hivi ningekuwa tu nimesoma darasani tu, na ningefikiri ni nadharia tu ya historia wala hakuna ukweli wowote .
Kwa sasa mpaka nafanya kazi na kujionea vitu mbali mbali vizuri siachi kuwashirikisha, na mimi ni balozi kwa sababu nimesoma masuala ya wanyamapori na nimetembelea maeneo mbali mbali ya wanyamapori na maeneo ya kihistoria. Hii ndio sababu nimeona nikushirikishe jambo hili muhimu; watu wengi baada ya kutembelea vivutio vya kitalii huwa wanawaambia na kuwaambiana mambo mazuri waliyoyaona kwa kwatu wengine.
Hivyo watanzania wnzangu na watu wengine tunatakiwa kujenga mabalozi wengi, tunatakiwa kuwa na ratiba kabisa ya kutembelea hifadhi na vivutio kwenye vyuo, shuleni na wakati mwingine hata makanisani na misikitini, tunaweza kuweka utaratibu wa kutembelea hifadhi za wanyama na vivutio mbali mbali ndani ya nchi yetu, hii yote ni kwa ajili ya kuitangaza Tanzania na kutengeneza utamaduni wa kufanya hivyo kwa jamii yetu.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 862 481/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania