Katika kuendelea kujifunza mambo mbali mbali kuhusu sheria ya wanyamapori namba 5. Ya mwaka 2009. Tutapata mwanga na kuelewa madhumuni na makusudi ya sheria hii ya wanayamapori. Leo tutajifunza kwa pamoja kwenye sehemu ya pili ya sheria hii, inayohusu, shabaha, nia na madhumuni ya sheria hii ya wanyamapori. Hivyo kwa mengi zaidi endelea kufuatilia mfululizo wa makala hizi.
5(1) Shabaha au nia ya sheria hii na kwa watu wote watakao kuwa watekelezaji, watumiaji au watafsiri wa sheria hii watawajibika au kufanya yafuatayo-
(a) Kulinda, kuhifadhi na kusimamia maeneo yenye mtawanyiko mkubwa wa viumbe hai, ikijumuisha maeneo oevu ambayo ndio sehemu zinazo wakilisha kwa kiasi kikubwa makazi ya wanyamapori na pia kuvipa uhifadhi maalumu kwa viumbe hai wanaopatikana eneo hilo tu, au kwa wanyamapori wachache, au spishi za wanyamapori ambao zipo hatarini kutoweka na kusaidia Tanzania kushiriki kikamilifu na kufaidika kutokana na juhudi za kimataifa na njia za kutunza na kuhifadhi viumbe hai duniani.
(b) Kulinda na kuhifadhi rasilimali za wanyamapori na makazi yao kwenye mapori ya akiba, maeneo oevu ya akiba, mapori tengefu, maeneo ya hifadhi ya jamii, maeneo yenye mtawanyiko wa wanyamapori na mimea, njia za mapitio ya wanyamapori, maeneo ya vizuizi vya asili, au maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kupunguza migogoro kati ya watu na wanyamapori wote wanaopatikana katika maeneo hayo, kwa kuweka miundombinu sahihi, watumishi wa kutosha na vitendea kazi;
(c) kuhamasisha na kuwezesha uchangiaji wa sekta ya wanyamapori kwa maenendeleo endelevu ya Tanzania na uhifadhi na usimamizi wa wanyamapori na maliasili kwa faida ya sasa na vizazi vya baadaye bila ubaguzi wowote;
(d) Kukuza na kuwezasha kukua kwa mifumo ya ikolojia ya wanyamapori sambamba na kuendeleza maeneo ya mtandao wa hifadhi ya wanyamapori kwa kusudi la kuwezesha uhifadhi wa mtawanyiko wa viumbe hai;
(e) Kuchangia, kuimarisha na kukuza mtandao wa maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori kwenye maeneo ya wanyamapori kama shughuli muhimu sana ya uhifadhi;
(f) Kuwezesha uhifadhi wa wanyamapori na makazi yake nje ya maeneo ya yaliyohifadhiwa kwa wanyamapori kwa kuanzisha maeneo ya hifadhi ya jamii, kwa kusudi la kuishirikisha jamii kwenye masuala ya uhifadhi;
(g) Kuhamasisha, kuinua na kurahisisha kuwepo na ushiriki hai wa jamii kwenye usimamizi endelevu, matumizi na kuhifadhi rasilimali za wanyamapori ndani na nje ya maeneo ya mtandao wa wanyamapor;
(h) Kuhakikisha uhifadhi wa wanyamapori unaendana na kukuwa kwa maendeleo vijijini kupitia kugawana majukumu ya usimamizi wanyamapori kwenye maeneo ya hifadhi ya jamii kwa wanajamii na kuhakikisha jamii inapata faida halisi na zinazoonekana kutokana na uhifadhi wa wanyamapori
(i)Kuhamasisha matumizi endelevu na yaliyo halali ya rasilimali za wanyamapori na kuchukua hatua stahiki kuzuia matumizi haramu au mabaya ya wanyamapori;
(j) Kusaidia kwa kiasi kikubwa watu wote au umma kupata taarifa na ufahamu kuhusu utamaduni, uchumi na faida za kijamii kwa kuhifadhi rasilimali za wanyamapori na kuwezesha kutambua mfumo wa uelewa wa wanajamii wenyeji kwenye uhifadhi wa wanyamapori na usimamizi na thamani halisi ya wanyamapori kwa jamii kwenye mipango ya usimamizi wa wanyamapori;
(k) Kupunguza migogoro baina ya watu na wanyamapori wakati wowote itakapotokea;
(l) Kutengeneza mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuwekeza kwenye namna mbali mbali za matumiza ya wanyamapori na uhifadhi na kutengeneza fursa kwa raia wa Tanzania kuwa washiriki kwenye sekta ya wanyamapori;
(m) kuiwezesha Tanzania kushiriki kwenye makubaliano ya kimataifa na kukuza sera katika msingi wa makubaliano sawaswa na nafasi ya Tanzania kwenye uhifadhi wa wanyamapori kwenye makubaliano hayo, na kushirikiana na nchi jirani katika uhifadhi wa mifumo ya ikologia inayounganisha nchi hizo.
(2) Kwa kusudi la kutoa mapendekezo yanayoathiri kifungu kidogo cha (l), mtu yeyote mwenye haki ya kuwa na ardhi kwenye eneo lililotangazwa kuwa pori la akiba atatakiwa kuwa na haki ya kulipwa fidia kama matakwa ya sheria kupata ardhi na sheria ya ardhi.
(6) mtu yeyote mwenye mamlaka ya kutumia sheria hii atatakiwa kuwa na wajibu wa kuikuza na kuiheshimu sera ya wanyamapori Tanzania.
Naamini kufikia hapa umepata kitu cha kukusaidia na pia umeelewa madhumuni, shabaha na nia ya uwepo wa sheria hii ya uhifadhi wa wanyamapori. Hivyo endapo hutaelewa vizuri usisite kuwasiliana nami, kwa sababu katika uchambuzi wa sheria hii ni kutoka kingereza kwenda Kiswahili, hivyo nimetumia muda mwingi kusoma na kuandika pole pole sana ili niandike kitu kinachoeleweka ili watu waelewe lengo, shabaha na nia ya sheria hii. Usiache kufuatilia mtandao huu kwenye makala ijayo tutaingia sehemu ya tatu ya sheria hii. Ambapo tutaangali mpangilio wa uongozi kwenye sekta hii karibu sana.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569