Habari za leo msomaji wa makala za Wildlife Tanzania, karibu tena kwenye makala zetu za kila siku ambapo tunajifunza na kuichambua sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009. Kuna mambo mengi sana yaliyopo ndani ya sheria hii ambayo kila mtu anapaswa kuyajua ili kujenga taifa lenye uelewa wa malisaili zake na rasilimali nyingine muhimu, na katika sheria hii tutajifunza na kuangalia sheria ya wanyamapori. Hivyo karibu sana kwenye makala hii ya uchambuzi wa sheria.

Kwenye makala iliyopita tuliishia kifungu cha 9 sehemu hii ya tatu ambapo ina vifungu vingine vidogo vidogo ambavyo nimevichambua taratibu ili tuweze kuielewa vizuri kwenye kila kipengele, leo tutaendelea na sehemu hii ya tatu kifungu cha 10 ambacho kinahusu uanzishwaji wa Idara ya Ulinzi wa wanyamapori, karibu twende pamoja.

10- (1) Waziri anaweza, baada ya kushauriana na mamlaka husika ambao zina wajibika na ulinzi na usalama na pia kwa ridhaa ya Rais, ataanzisha Idara ya Ulinzi ambayo itaitwa Iadara ya  Ulinzi wa Wanyamapori (Wildlife Protection Unit). Kwa hiyo tunaona hapa mwenye mamlaka ya kuunda na kuanzisha Idara ya  ulinzi wa wanyamapori ni waziri mwenye dhamana, waziri wa maliasili na utalii ndie anayeweza kuanzisha kikosi hicho kwa ridhaa ya Rais wa nchi na mamlaka husika,  Idara hii mara nyingi ni askari wanyamapori ambao hufunzwa na kuandaliwa maalumu kwa kazi hiyo.

SHUGHULI ZA IDARA YA ULINZI

Kwa mujibu wa sheria hii kifungu cha 11, uanzishwaji wa idara ya ulinzi wa wanyamapori utakuwa unashughulika na ulinzi wa wanyamapori dhidi ya ukiukwaji wa sheria ya matumizi yanayohusiana na uwindaji, ukamataji na upigaji picha na kuhakikisha usalama wa  nyara za serikali.  Hivyo basi masuala yote yanayohusu usalama wa wanyamapori unasimamiwa kisheria na idara hii kuu ya ulinzi, ni idara nyeti na muhimu sana kwenye uhifadhi na usalama wa wanyamapori.

UONGOZI/USIMAMIZI WA IDARA YA ULINZI

Katika kuhakikisha kunakuwa na uongozi na usmamizi kwenye idara hii, sheria imeweka madaraka yote ya uongozi na usimamizi wa idara hii kwa mkurugenzi na kwa makusudi hayo idara itaundwa kikanda na watapanga kulingana na maeneo au sehemu kama mkurugenzi atakavyo nuia. Hivyo uongozi na usimamizi wa idara hii utakuwa chini ya mkurugenzi wa wanyamapori na pia idara hizi zitakuwa zinafanya kazi kikanda kwenye maeneo au sehemu ambazo mkurugenzi atakuwa amepanga.

(2) Wazira mwenye dhamana ata, baaada ya kushauriana na mamlaka husika ambazo zinawajibika kwa ulinzi na usalama na pia kwa ridhaa ya Rais na kwa mapendekezo katika Gazeti la serikali atandaa yafuatayo-

(a) ataunganisha na kupanga idara, kwa masharti na vigezo vya huduma kwenye madaraja mbali mbali na kufanya uteuzi; hapa sheria inampa ruhususa kuwapandisha cheo  baadhi ya askiri wanaostahili, pia atafanya uteuzi mbali mbali ndani ya idara ya ulinzi wa wanyamapori.

(b) majukumu ambayo yanatakiwa kufanywa na mwana idara, na maelekezo na namna ya kuondoa majukumu hayo;

(c) Utaratibu/ kanuni za mambo yote yanayohusiana na nidhamu kwenye Idara;

(d) maelezo, utumiaj, kumiliki wa risasi, vifaa vidogo vidogo, sare za askari, na mahitaji maengine muhimu kwa wafanyakazi wa idara ya uilinzi;

(e) mambo yote ya jumla yanayohusiana na kufuata utaratibu mzuri na uongozi au usimamizi wa idara.

Naamini kwa kufikia hapa tumepata kitu cha kusaidia kuijua sheria hii, kwenye makala ijayo tutajifunza umiliki wa silaha za moto, bunduki, risasi na jinsi sheria ilivyo wazi kwenye idara hii ya ulinzi wa wanyamapori.

Ahsante sana kwa kusoma makala hii, tuendelee kuwa pamoja kwa makala ijayo, pia mjulishe au mshirikishe Rafiki yako maarifa yaha

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 248 681/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania