Habari msomaji wa mtandao huu wa Wildlife Tanzania, karibu tena kwenye mfululizo wa makala za uchambuzi wa sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009. Jana tulimaliza sehemu ya tano ambayo ilikuwa na mambo mazuri kuhusu uanzishwaji na usimamizi wa maeneo ya hifadhi ya jamii. Leo tunaendelea na sehemu ya sita ambayo pia ni muhimu sana kwani inalelezea  mpango wa jumla wa usimamizi na uandaaji wa mpango wa jumla wa usimamizi wa wanyamapori na maliasili nyingine kwenye maeneo ya hifadhi ya jamii. Leo tunaendelea na kifungu cha 34 katika sehemu hii ya sheria ya wanyamapori , hivyo karibu twende pamoja.

34.-(1) Mkurugenzi ataanzisha, mapema kama iwezekanavyo, baada ya uanzishwaji wa maeneo ya hifadhi ya wanyamapori, ataandaa na kusababisha kuwepo kwa Mpango wa Jumla wa Usimamizi wa kila eneo la hifadhi ya wanyamapori.

(2) Kila Jumuiya yenye mamlaka itaandaa, baada ya uanzishwaji wa Eneo la Usimamizi wa wanyamapori, Mpango wa Usimamizi wa  Maliasili wa Kanda (Resource Management Zone Plan) kabla ya kupewa haki ya matumizi ya maliasili kwa kipindi cha majaribio kabla ya Mpango wa Jumla wa  Usimamizi hauijatumika.

(3) Mpango wa Jumla wa Usimamizi unatakiwa kuandaliwa kwa mfumo wa ushrikishwaji na unatakiwa kuwa na taarifa ambazo zimeelezwa kwenye sheria husika.

(4) Waziri anatakiwa kuhakiki na kuchapisha Mpango wa jumla wa usimamizi kwenye Gazeti la serikali.

(5) Mipango yote na hatua zote zinatakiwa ziende sawa a maelekezo yaliyoelezwa kwenye mpagp husika wa usimamizi kwa eneo husika.

(6) Mango wa Jumla wa Usimamizi unatakiwa kufanyiwa mapitio au marejeo kwa kipndi fulani au kuifanya iendane na wakati kulingana na kanuni zilizotungwa kwenye Gazeti la serikali na Waziri.

35.- (1) Kila mradi au ujenzi maendeleo yoyote ndani ya eneo la hifadhi ya wanyamapori, kwenye Eneo la Hifadhi ya Jamii, kwenye eneo linalopunguza athari,au eneo la amani (Buffer Zone), Njia ya Mapitio ya wanyamapori, ambayo sehemu hii ya sheria inatumika, haijalishi maendeleo hayo yameandaliwa na, au yanatekelezwa na mtu au kampuni katika sekta ya umma au sekta binafsi, muhusika wa mradi huo anatakiwa kuandaaa na kuwasilisha kwa Waziri anayehusika na mazingira ripoti ya Tathimini ya Athari za Mazingira (Environmental Impact Assessment) ya mradi unaokusudiwa.

(2) Licha ya kifungu kidogo (1) au sheria nyinyinge ambayo ni tofauti, mradi au ujenzi wowote ambao sehemu ya kifungu hiki inatumika hautaanza isipokuwa na mpaka cheti cha Tathimini ya Athari za Mazingira kimetolewa na Waziri anayehusika na mazingira. Hapa anamaanisha endapo kutakuwa na mradi unaotaka kufanyika kwenye maeneo ya hifadhi za wanyamapori, vigezo na masharti yote ya sheria hii yanatakiwa kutumika, kama ni kutafuta cheti cha athari za mazingira ni lazima izingatiwe na kufanyika kwa mujibu wa sheria hii.

(3) Ujenzi wowote kwenye maeneo ya hifadhi ya wanyamapori na kwenye maeneo ya hifadhi ya jamii ambayo sehemu hii ya kifungu cha sheria inatumika itajumuisha shughuli kama-

(a) uchimbaji wa madini;

(b) ujenzi wa barabara au kuchimbia mabomba ya mafuta

(c) Ujenzi wa muda au ujenzi wa muda murefu;

(d) ujenzi wa mabwawa, vituo vya umeme, kuweka  miundombinu ya umeme na mawasiliano na;

(e) ujenzi mwingine unaofanana au shughuli nyingine kama Mkurugenzi atakaruhusu kwa nia njema au atashauri

(4) Namna na kiini cha kila Tathmini ya Athari za Mazingira ambayo sehemu hii ya sheria inatumika inatakiwa kuwa sawa na matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, na inatakwa kuzingatia na kufanya kila kitu kwa ubora wa kimataifa.

(5) Tathimini ya Athari za Mazingira zitakazofanyika kulingana na kifungu kidogo cha (4) itajumuisha athari zitakazoletwa kwa wanyamapori na itatakiwa kutoa au kuandaa

(a) kauli ya jumla ya kutokea au matarajio ya athari za kiuchumi kwenye uhifadhi wa wanyamapori, ikijumuisha spishi, jamii na makazi yatakayoathirika na kiwango kitakachopelea tishio la viumbe hai

(b)Kauli ya jumla kama kuna wanyamapori adimu au wapo kwenye tishio na inayoonyesha spishi ambazo ni za eneo hilo tu na makazi yao na kama zinaweza kuathirika;

(c) orodha ya njia mbadala  pamoja na hatua za kuchukua kuzuia au kukabiliana na  athari mbaya ambazo zinaweza kutumika kuondoa  athari mbaya; na

(d) mapendekezo ya hatua za kuchukua baadaye.

(6) Mkurugenzi anaweza, baada ya kushauriana na mamlaka na taasisi husika ataandaa maelekezo yaTathimini ya  Athari za Mazingira (Environmental Impact Assessment guidelines).

(7) Katika utendaji wa majukumu yake katika sehemu hii ya kifungu cha sheria, Mkurugenzi anaweza kushauriana na mtu, mamlaka, taasisi na kampuni ambazo zinaweza kuwa zinahusika kwa namna moja ama nyingine.

(8) Baada ya kukubaliwa kwa Athari za mazingira na mamlaka zinazowajibika au makampuni,Tathimini ya Athari za Mazingira itatakiwa kuunganishwa na mradi huo.

  1. Mkurugenzi anaweza kufanya ukadiriaji au tathimini ya athari watakazopata wanyamapori sehemu ambayo kuna mradi unafanyika sawa na kifungu cha 34 au shughuli yoyote inayofanyika kama inaweza kuwa na madhara mabaya kwa spishi za wanyamapori, jamii na makazi yao
  2. Mkurugenzi ataruhusu mamlaka husika kufanya ufuatiliaji na ukaguzi wa mazingira kwa miradi au shughuli zinazofanyika kwa mujibu wa sheria hii ikijumuisha yote ambayo yalifanyika kabla ya matumizi ya sheria ya usimamizi wa mazingira.

Namini hadi kufikia hapa tunaweza kuelewa mpango mzima wa uendeshaji wa shughuli mbali mbali ndani ya hifadhi za wanyamapori. Endelea kufuatilia sheria hii.

Ahsante sana!

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 248 681/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania