Gharama za uendeshaji na usimamizi, vifaa na nguvu kazi kwenye kuhakikisha shughuli za uhifadhi wa wanyamapori zinafanyika vizuri na kwa ufanisi huwezi kutaja na kufanya vitu hivyo vyote bila kuwa na Fedha za uhakika. Kati ya changamoto kubwa kwenye sekta ya wanyamapori ni kutokuwa na fedha za kutosha kukamilisha au kuendesha shughuli za kiuhifadhi. Kwa kutambua hilo serikali ikaamua kuweka Mfuko wa Hifadhi ya wanyamapori Tanzania ambao utasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazohitaji fedha, huu ni mfuko wa kudumu na unaopata fedha kutoka katika vyanzo mbali mbali kama itakavyoeleza kwenye uchambuzi wa sehemu hii ya Kumi na Tatu ya sheria namba 5 ya mwaka 2009.
Hivyo mfuko huu ambao umeanzishwa na kusimamiwa kisheria ni muhimu sana kwa ajili ya kuhakikisha kunakuwa na rasilimali fedha na mali nyingine muhimu zenye msaada kwenye suala zima la uhifadhi wa wanyamapori Tanzania. Ni mfuko salama na unasimamiwa na watu wenye sifa na wenye uzoefu kwenye masaula ya uhifadhi wa wayamapori na mambo ya fedha na uchumi. Karibu tujifunze kwa pamoja sehemu hii muhimu ya sheria.
- (1) Utaendelea kuwepo Mfuko unaojulikana kama Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania au kwa lugha ya kingereza uinaitwa Tanzania Wildlife Proctection Fund na kifupisho chake kinajulikana kama “TWPF”.
(2) Madhumuni ya Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania itakuwa ni kurahisisha na kusaidia uhifadhi wa wanyamapori, ndani na nje ya maeneo yaliyo hifadhiwa hasa-
(a) kwenye shughuli au operesheni dhidi ya ujangili na utekelezaji wa sheria;
(b) kwenye opareshini za Idara ya Ulinzi wa wanyamapori;
(c) kwenye uhifadhi wa wanyamapori;
(d)kuendeleza jamii ambazo zinaishi karibu na maeneo ya hifadhi za wanyamapori;
(e) kutoa elimu ya uhifadhi, mafunzo, na kuteneneza uelewa na ufahamu kwa jamii kuhusu masuala ya wanyamapori;
(f) kujenga uwezo kwenye masuala ya usimamizi wa wanyamapori;
(g) kusimamia utafiti wa wanyamapori; na
(h) shughuli yoyote inayohusiana na uhifadhi wa wanyamapori.
(3) Vyanzo vya mapato ya mfuko itajumuisha-
(a)kiasi cha fedha ambacho kinaweza kuidhinishwa au kutengwa na Bunge;
(b)asilimia ishirini na tano (25%) ya mapato ya kila mauzo ya mnyama, nyara, silaha, magari, boti au meli, ndege,mahema, au kitu kingine chochote ambacho kimetwaliwa na kushikiliwa kwa kifungu kidogo cha 110 cha sheria hii na kuuzwa au kuhifadhiwa na kwa namna ambayo fedha ikijumuisha mapato yaliyokusanywa kutokana na yasiyo matumizi ya matuizi ya wanyamapori nje ya hifadhi za Taifa na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro;
(c) jumla ya fedha au mali ambayo kwa kila nmna inaweza kuwa inaitajika kwa ajili ya kuweka kwenye Mfuko; na
(d) kiasi chochote kinachotakiwa kulipwa au michango, misaada na ufadhili uliofanywa au uliotolewa na kuwekwa kwenye Mfuko kwa mawakala,taasisi, watu binafsi na hata misaada ya serikali za nchi nyingine au mashirika ya kiimataifa.
(4) Waziri anaweza kuunda kanuni kwenye Gazeti la Serikali kuweka usimamizi, majukumu na matumizi ya Mfuko, na pia baada ya kushauriana na Waziri anayehusika na masuala ya fedha, ataunda kanuni kwenye Gaezti la Serikali kwa ajili ya uendeshaji wa Mfuko.
92.-(1) Kutaanzishwa Bodi ambayo itajulikana kama Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania ambayo –
(a) itaendelea kudumu na kuwa na muhuri wa pamoja;
(b) kwa jina lake la shirika itakuwa na uwezo wa kushitaki au kushitakiwa; na
(c) itakuwa na uwezo wa kufanya manunuzi, au kupata na kusimamia chochote na kunyang’anya mali yoyote inayohamishika na isiyohamishika.
(2)Bodi itakuwa na uwezo wa kushikilia, kufanya manunuzi, au kwa namna nyingine kupata mikataba ya hazina (treasury bond), kunyang’anya mali yoyote inayohamishika na kwa ridhaa ya Waziri, mali yoyote isiyohamishika kwa kusudi la majukumu au shughuli zozote zilizotolewa na Bodi kwa sheria hii.
(3) Bodi itajumuisha wafuatao-
(a)Mwenyekiti ambaye atateuliwa na Rais, na ambaye ni
(i)msomi wa chuo kikuuu kinachojulikana; na
(ii)mtu ambaye ameonyesha uwezo, uaminifu na uzoefu kwenye shughuli za umma inaweza kuwa mambo ya wanyamapori, uchumi, sheria, usimamizi au mambo mengine yanayohusiana;
(b) muhifadhi wa Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro;
(c) Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania;
(d)Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti yaw a Wanyamapori Tanzania;
(e) Wakili Mkuu wa Serikali aliyeteuliwa na Mwanasheria Mkuu wa kwa niaba yake;
(f) Muhasibu Mkuu anayemwakilisha Waziri wa Fedha;
(g) wajumbe wawili wenye uwezo, uaminifu, uelewa na uzoefu kwenye masuala ya uhifadhi wa wanyamapori walioteuliwa na Waziri;
(h)Mkurugenzi atakuwa ndiye Ofisa Mtendaji Mkuu (Chief Exacutive Officer) na katibu Mkuu wa Bodi.
(4) Mkurugenzi anaweza kunaibisha mamlaka yake kwa meneja wa Mfuko.
(5) Bodi itakuwa na nguvu ya-
(a)kuingia mikataba;
(b)kukubali au kukataa mipango ya uwekezaji na miradi; na
(c) kufanya shughuli nyingine kwa ajili ya kuboresha utendaji wa shughuli zake chini ya sheria hii.
(6) Shughuli za Bodi zitakuwa-
(a)kusimamia na kuendesha Mfuko kwa mujibu wa Sheria hii; na
(b)kulingana na Sheria hii na maelekezo yoyote yaliotolewa na Waziri, kufanya kitendo au kitu chochote kwa ajili ya kutangaza kwa kusudi na madhumuni ya Mfuko.
(7) Muda wa ofisi na vikao na mambo yote ya kiutaratibu ya Bodi yatawekwa kwenye Jedwali la Sita la Sheria hii. Ufafanuzi kidogo hapa ni kwamba kuna muda ambao bodi itaongoza au kuwa madarakani, muda huo ni miaka mitatu, baada ya hapo wanateua wajumbe wengine. Hii ni kwa mujibu wa Jedwali la Sita (Six Schedule) la Sheria hii.
(8) Waziri, baada ya kutoa taarifa kwenye Gazeti la Serikali, ataandaa kanuni za utendaji na uendeshaji na za kiushauri pamoja na mambo mengine yanayohusiana na Bodi.
93.- (1) Mfuko utatunza vitabu vya mahesabu na kusimamia vizuri kumbukumbu za utendaji wake kwa mujibu wa viwango vinavyokubalika vya mahesabu.
(2) Mkurugenzi atahakikisha, kwa muda wowote, na mwisho wa mwaka wa fedha mahesabu ya mfuko yamekaguliwa na kupitiwa na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali.
(3)Mkurugenzi anatakiwa kuwasilisha taarifa ya ukaguzi chini ya kifungu kidogo cha (2) pamoja na taarifa ya mwaka ikionyesha kwa kina taarifa kuhusiana na shughuli za Mfuko kwa mwaka uliopita unaoishia tarehe 30 Juni kwa waziri.
(4) Waziri ataiweka mezani taarifa ya ukaguzi kwenye mkutano Mkuu wa Bunge.
Huu ndio mfuko wa fedha unaoendesha shughuli za uhifadhi wa wanyamapori kwenye maeneo mbali mbali. Naamini kabisa umeelewa jinsi mfuko huo ulivyoanzishwa unavyoendeshwa na vyanzo vya mapato pamoja na mambo mengine mengi ya kiuwajibikaji yaliyowekwa kwenye mfuko huu kwa mujibu wa sheria ya wanyamapori Tanzania. Ni mfuko wenye manufaa sana kwani unatoa suluhisho kwenye mambo mengi ya kiuongozi, usimamizi na kitaaluma. Hivyo ni mfuko ambao upo kisheria na unasimamiwa kisheria na watu wenye sifa na weledi kama walivyotajwa kwenye sheria hii.
Ahasante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania