Katika kujifunza na kuhakikisha tunapata uelewa mpana wa masuala ya uhifadhi wa wanyamapori nilipitia na kusoma makala hii iliyoandikwa na Ripple na wenzake nimeamua nikushirikishe niliyojifunza kutoka kwenye makala yake aliyoichapisha mwaka 2017, ambayo inaitwa Conserving the World’s Megafauna and Biodiversity: The Fierce Urgency of Now, kwa kuwa nimekosa maneno ya moja kwa moja ya Kiswahili ya kutafsiri kichwa cha makala yake nimejaribu kuweka kichwa ambacho kinaendana na cha makala yake, hivyo karibu usome ujipatie maarifa muhimu.

Hivyo msomaji wa makala hizi za wildlife Tanzania leo nimekuletea mambo machache ambayo nimejifunza kutoka kwenye makala hii ya uhifadhi wa wanyamapori wanaoishi au wanaotegemea maeneo makubwa ya hifadhi, ili waishi wanamchango mkubwa sana kwenye kuhifadhi na kuendelea kwa viumbe hai wengine. Hivyo nimeamua nikushirikishe baadhi ya mambo muhimu niliyojifunza kutoka kwenye makala hii iliyoandikwa kwa kingereza. Hivyo karibu fuatana nami ili tujifunze kwa pamoja kwa ajili ya maliasili zetu.

Wanyamapori wakubwa wnaokula nyama na wanaokula majani ni wanyama ambao wapo kwenye tishio la kutoweka kwenye uso wa dunia, hivyo juhudi za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa mapema sana kabla ya hali hii haijawa mbaya zaidi ya hapa, tunahitaji utekelezaji wa haraka wa mipango na mikakati ya kunusuru wanyama hawa ambao ndio kiini cha uhifadhi na uwepo wao unahakikishia wanyama na viumbe hai wengine mazingira ya kuishi. Wala hili la kuhifadhi wanyama hawa haina maana kuwa wengine hawana umuhimu, lakini tafiti za kimazingira na ikologia zinasema endapo wanyama hawa wakubwa au wanyama hawa wanao hitaji maeneo makubwa kwa ajili ya kuishi watahifadhiwa basi kazi itakuwa ndogo sana kwenye kuwahifadhi wanyama na viumbe hai wengine.

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 1970 hadi 2012, uchambuzi uliofanyika duniani unaonyesha kupungua kwa asilimia 58 ya wanyamapori hawa, hivyo tunawajibu kama dunia kuhifadhi asilimia ya wanyamapori waliobaki, hii ni pamoja na kuwa tayari kuanzisha njia mbali mbali za kuhifadhi na mbinu mbali mbali za kuhakikisha idadi ya wanyama hawa zinzendela kuwepo na kuongezeka zaidi hapa duniani.

Ni ukweli usio pingika kwa wanyama hawa wanaishi sehemu kubwa ya hifadhi au pori kubwa wanakuwa ni kama mwavuli kwa viumbe wengine kuishi ha kuendelea kuwepo wake kwenye maeneo hayo utachangia sana utunzaji wa mazingira na makazi ya viumbe hai wengi sana. Hivyo kwa kuwa wanyama hawa huitaji maeneo makubwa kuishi, hivyo maeneo mengi ya makazi ya viumbe hai yatatuzwa kwa kutunza wanyamapori hawa.

Maeneo yenye utajiri mkubwa wa viumbe hai (biyoanuai) duniani yanatofautiana, mengine yana idadi kubwa kuliko nchi nyingine. Hivyo nchi ambazo zina idadi kubwa ya maeneo hayo yenye utajiri wa viumbe hai yanapaswa kulindwa kwa gharama kubwa sana. Maeneo hayo yenye idadi kubwa sana ya bioanuai duniani yanapatikana katika nchi 17 tu dunia nzima, hivyo sisi kama watu ambao tumejaliwa kuwa na idadi kubwa ya viumbe hai tunatakiwa kuwajibika zaidi ili tupate msaada kutoka kwa wadau wengine wa maliasili duniani. Hivyo kutokana na hali hiyo uhifadhi na nguvu kubwa sana imewekwa kwenye maeneo haya yenye idadi kubwa sana ya bioanuai.

Endapo wanyama hawa watauliwa na kupungua itasababisha mabadiliko mabaya kwenye ikologia ya wanyamapori wengine na viumbe hai wengi, pia itawaathiri wanyamapori wadogo waliopo kwenye maeneo husika. Wanyama hawa ni muhimu waendelee kuwepo na kusaidia maazingira kubaki kwenye hali yake ya uasili, wanyamapori unaozungumzia hapa ni wale walao nyama wakubwa kama vile simba, chui, duma, mbwa mwitu, fisi, na wale wanao kula majani ni kama vile tembo, twiga,  pundamilia, na wngine wengi, ni muhimu sana tukatilia mkazo kwenye kuhakikisha usalama wao.

Asante sana kwa kusoma makala hii.

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

0742092569/0683248681

hillarymrosso@rocketmail.com