Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania! Naam, kazi iendelee! Asanteni sana. 

Siku ya Askari Wanyamapori duniani kila tarehe 31July

Kila mwaka, tarehe 31 Julai  ni siku ya Askari Wanyamapori duniani, ndio ni siku ambayo tunasharekea, kuenzi na kukumbuka mchango mkubwa askari wetu walio jeruhiwa, kuumizwa na waliopoteza maisha katika harakati za usimamizi wa maliasili zetu.

Naelewa kwanini dunia iliamua kutambua umuhimu wa askari wa wanyamapori  na kuweka siku moja maalumu kwa ajili ya kuwaenzi na kutambua mchango wao mkubwa katika usimamizi wa rasilimali zetu.

Rasilimali tulizonazo hapa duniani zinaelekea kupungua na kupotea kwa kasi kubwa sana kutokana na usimamizi dhaifu unaochangiwa na mambo mengi sana kama vile, uporaji, ujangili, umasikini, rushwa, magonjwa, na siasa zisizo rafiki nk. Hivyo kumekuwa na kukithiri kwa vitendo vya kihalifu dhidi ya maliasili zetu.

Maliasili hapa namaanisha, uoto asilia, madini, wanyamapori, misitu, vyanzo vya maji, na bahari. Rasilimali zote hizi zimeathiriwa sana na mienendo mibaya ya maisha ya binadamu juu ya uso wa nchi, shughuli za maendeleo ambazo kwa kiasi kikubwa zimechangia kuharibika kwa maeneo mengi asilia ambayo ni makazi muhimu ya viumbe hai, na mifumo muhimu ya ikolojia, uchafuzi wa mazingira na vyanzo vya maji kumepelekea kupotea kwa kiasi kikubwa cha rasilimali na viumbe hai wengi wa majini na nchi kavu.

Kutokana na hali hii, nchi zetu na dunia kwa ujumla zikaamua kuwepo kwa askari wa wanyamapori, ambao pamoja na mambo mengine washirikiane na jamii na taasisi au sekta nyingine katika ulinzi na usimamizi wa wanyamapori na rasilimali nyingine asilia. Hata hivyo, askari wanyamapori au Rangers wanafanya majukumu mengine mengi sana kama vile kutoa elimu kwa jamii kuhusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira, kushiriki katika shughuli za kiutafiti, kutatua migogoro ya watu na wanyamapori, kuzima mioto na kufanya kazi nyingine za kiikolojia ndania na nje ya hifadhi.

Usimamizi wa rasilimali hizi hujawahi kuwa  kazi rahisi hata siku moja, hii ni kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kijangili katika ngazi za kitaifa na kimataifa, ukubwa wa maeneo ya usimamizi, kukosekana kwa vifaa vya kisasa  na vitendea kazi vya kutosha, rushwa maeneo ya usimamizi, biashara ya wanyamapori na nyara, ongezeko la mifugo na uvamizi wa maeneo asilia kwa ajilia makazi na kilimo, siasa zisizo rafiki katika uhifadhi wa maliasili, bajeti isiyotosheleza usimamizi na uendeshaji wa shughuli za uhifadhi, maslahi madogo, magonjwa kama HIV/AIDS na COVID-19, kwa kiasi kikubwa vimechangia sana kufanya shighuli za usimamizi wa maliasili hizi kuwa mgumu kwenye maeneo mengi ya Afrika na Tanzania ikiwepo.

Picha hii imetolewa katika website tarehe 31 July, 2021https://www.tusk.org/events/wildlife-ranger-challenge-2021/

Hata hivyo, askari wetu wa wanyamapori wamekuwa wakaifanya kazi kubwa sana licha ya uwepo wa changamoto zote hizo. Wengi wamekuwa msitari wa mbele katika harakati za ulinzi wa maliasili hizi, wengi wamepata vilema na kuuwawa na majangili na wanyama wakali katika shughuli zao za usimamizi wa wanyamapori.

Hivyo, katika kuadhimisha siku hii muhimu ya duniani, nimeandika makala hii kwa kuheshimu,kutambua umuhimu na  mchango wao mkubwa katika uhifadhi na usimamizi wa rasilimali hizi muhimu kwa ajili yetu na kwa ajili ya vizazi vingi vijavyo.

Ningependa serikali iongeze uwekezaji katika sekta hii muhimu kwasababu ndio sekta inayochangia katika kukuza uchumi na kuchangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa. Uwekezaji mkubwa uende katika kuboresha ufanisi na kuongeza motisha kwa askari wetu wanaofanya kazi hizi ngumu za uhifadhi wa wanyamapori.

Mwisho, niwapongeze askari wanyamapori kwa kuendelea kufanya kazi zao kwa weledi licha ya changamoto nyingi. Pia niipongeze serikali na wadau wengine wanaochangia katika kuboresha na kuwekeza katika sekata hii muhimu kwa kuwasaidia askari wetu vitendea kazi, mafunzo na ujuzi katika harakati za kulinda na kusimamia maliasili zetu. Juhudi hizi ziendelee ili kulinda afya, usalama wa askari wetu na maliasili zetu.

Kila la kheri Asakri wetu katika majukumu yenu!

Happy World’s Rangers day!

Imeandikwa na Hillary Mrosso

hillarymrosso@rocketmail.com

+255 742 092 569