Kuna sehemu nyingi sana ambazo unaweza kwenda na familia yako, na kuna sehemu nyingine hauwezi kwenda na familia yako, kunamaeneo ambayo unatamani kwenda mwenyewe, kuna maeneo ambayo hutamani mtoto wako aende. Lakini kwenye maeneo ya hifadhi za wanyama na vivitio vingine unatakiwa kujua kuwa mtoto wako naye anatamani kujua na kuelewa kuwa vitu vya aina hii vipo na vinapatikana Tanzania.
Kuna vitu vingi ambavyo watoto hawajui kwenye maisha yao, hivyo ni kazi ya mzazi kuamua kumsaidia mtoto kuwekeza vitu hivyo kwenye akili yake. Unapomtebeza mtoto maeneo mbali mbali hata akili yake na uwezo wake wa kufikiri unaongezeka. Ataanza kufikiria vitu vipya kwenye akili yake ataanza kuwa na matamanio ya kufanya vitu vipya alivyo viona kwenye maisha yake. Hivyo kuwapa watoto nafasi ya kutembelea sehemu mbali mbali zenye vivutio itawajenga sana.
Pia kwa kufanya hivi tunajenga kizazi chenye uzalendo na kujali maliasili za nyumbani, hivyo wazazi sehemu nzuri ya kuwaruhusu watoto wako kwenda mara kwa mara wanapopata nafasi ni maeneo ya hifadhi ya wanyama, sehemu za vivutio nan k. usiwaache tu watoto wako wavione vitu hivyo kwenye TV pekee watengenezee utaratibu wa kuviona kwa macho yao wenyewe.
Kuna watoto wengine hawataonyesha wana vipaji gani mpaka umpeleke kwenye mazingira fulani, au aone vitu fulani vinafanyika, kwa mfano mimi mwenyewe nilikuwa sijui kama kuna kozi za wanyamapori na kama inawezekana kusoma na kufanya kazi kwenye sekta hii, mpaka pale nilipoanza kuona na kusoma kwenye magazeti ya kakakuona kuhusu wanyamapori. Hapo ndipo nilipovutiwa sana na wanyamapori na kuamua kuacha kusomea udaktari na kuamua kwenda kwenye wanyamapori. Hivyo naamini hata watoto tulio nao wanaweza kuwa na matamanio mbali mbali na ndoto bali mbali lakini akienda maeneo tofauti tofauti atajifunza na kuona vitu vipya ambavyo vitampa maono na ndoto yake itatimia.
Asante sana kwa kusoma makala hii,
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 862 481/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania