Habari Rafiki, naamini unaendelea vizuri na ratiba zako za kila siku, karibu kwenye makala zetu za kila siku kuhusu uchambuzi wa sheria ya wanyamapori Tanzania, bila shaka tupo kwenye sehemu ya saba ya sheria hii ya wanyamapori ambayo kwa kiasi kikubwa sehemu hii ya sheria imejikita kwenye matumizi na ambayo sio matumizi kwa maliasili za wanyamapori. Tukiangalia kwa jicho la kitalii tunasema utalii wa uwindaji na utalii wa picha, masharti, lesseni , vibali na kanuni za sheria inayosimamia shughuli nzima za matumizi ya wanyamapori, mamlaka ya Mkurugenzi na pia mamlaka ya Waziri kwenye maeneo mbali mbali ya vipengele vya sheria hii muhimu. Karibu tuendelee nauchambuzi wetu ambao unaanza katika kifungu cha 59.

Katiaka sehemu ya kuanzia tutaanza na kipengele ambacho kinasema ulinzi wa kisheria kulingana na sheria hii au tunaweza kusema usalama kwa mtekelezaji wa sheria hii.

  1. – (1) Mkurugenzi anaweza, kama masharti ya utaoaji wa lesseni yoyote au kibali kwa mujibu wa Shaeria hii, kuelekeza kwamba mwombaji atapewa ulinzi kwa kuzingatia matakwa ya sheria hii na sheria nyingine ndogo zilizotungwa pia kwa kuweka pamoja na Mkurugenzi kiasi cha fedha ambacho sio chini ya thamani ya mnyama, au isizidi mara mbili ya thamani yake au sawa na makubaliano ya udhamini au bila udhamini kwa kiasi cha zaidi ya mara mbili ya thamani ya mnyama au wanyama, kama Mkurugenzi atakavyo azimia.

(2) Mtu yeyote ambaye amepewa ulinzi kwa mujibu wa kifungu cha sheria hii, akikiuka kipengele chochote cha sheria hii au sheria nyingine ndogo kwa muda wa miezi tisa baada ya ulinzi huo kutolewa, kwa hiyo, licha ya adhabu na penati ambazo atakuwa nazo au atapewa muhusika ambaye amekiuka masharti ya kipengele hiki cha sheria-

(a) wkati kiasi cha fedha kimewekwa pamoja na Mkurugenzi, kiasi hicho cha fedha, au sehemu ya fedha hiyo Mkurugenzi anaweza kwa maandishi ya moja kwa moja, kuipeleka na kuikabidhi kwa serikali kama adhabu ya kutotii sheria au kuvunja sheria hii.

(b) pale makubaliano ya udhamini yatakapofanyika,  makubaliano hayo ya kimaandishi yatatakiwa kutekelezwa na Mkurugenzi kwa niaba ya Serikali, sambamba na kiasi chote kilichotajwa kwenye makubaliano au sehemu ya kiasi ambacho Mkurugenzi atakianisha kwa maandishi.

60.- (1) Mtu hatatakiwa kuhamisha au kumpa mtu mwingine yeyote lesseni  kibali au mamlaka yoyote ya kimaandishi (kibali chochote cha maandishi) kilichotolewa kwa mujibu wa Sheria hii. Kwa ufafanuzi hapa ni kwamba endapo wewe ndiye mmiliki wa lesseni au kibali chochote cha matumizi ya wanyamapori, sheria inasema huwezi kumpatia au kumwachia mtu mwingine lesseni au kibali chako akitumie badala yako kwa shughuli za matumizi ya wanyamapori na maliasili. Kuna utaratibu mzuri wa sheria wa kufanya hivyo.

(2) Mtu yeyote ambaye anatafuta kuhamisha au kumpa mtu mwingine leseni, kibali au mamlaka ya kimaandishi atatakiwa kuomba kwa maandishi kwa Mkurugenzi akieleza sababu za kutoa au kumpa mtu mwingine lesseni au kibali chake.

(3) Waziri anaweza, kwa kufuata kanuni kwenye Gazeti la serikali, kuelezea masharti ya kuhamisha au kutoa lesseni yoyote kwa mtu mwingine sawa na sehemu ya (2) ya sheria hii.

(4) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kifungu hiki cha sheria anafanya kosa na atatoa faini isiyopungua shilingi milioni tano au kifungo jela kisichopungua mwaka mmoja na kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Naamini kwa vifungu vichache tulivyochambua hapo utaelewa baadhi ya mambo ya msingi kwenye sheia hii. Kumbuka hili siku zote kutoifahamu sheria sio kisingizio cha kukiuka na kufanya kinyume na sheria hiyo. Kwenye ulimwengu wa sheria kuna Imani kwamba kila mtu anaifahamu sheria ipasavyo, hivyo kwa kutokujua sheria na kufanya kosa utahukumiwa sawa na sehemu ya sheria uliyokiuka na kuivunja. Ndio maana nakushauri ujifunze kidogo kidogo mambo haya ya sheria hasa kwa wafanyakazi na watu wanaotaka kuwekeza kwenye sekta hii ya wanyamapori.

Tukutane hapa Kesho kwa makala nyingine!

Asante sana!

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 248 681/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania