Habari Rafiki, karibu sana kwenye makala ya leo tujifunze na kujadili kwa pamoja vitu vidogo vidogo ambavyo vinatokea kwenye sekta ya maliasili na utalii vinavyoweza kusababisha madhara makubwa kwa hali na mwenendo wa baadaye kenye sekta hii. Ni vizuri tukawaza na kuwazua ili kuweka kila kinachowezekana, kufanya kila kinachowezekana kufanyika kwa nia njema ya kunusuru urithi wa rasilimali tulizopewa na Mungu kwa ajili ya usimamizi mzuri.

Huwa kuna wakati nawaza sana kama watu ambao Mungu ametuamini na kuamua kutupa utajiri wa kila aina ili tuutumie na kuusimamia kwa ajili ya makusudi yake mwenyewe. Lakini pia huwa nafikiria pale ambapo tuanashindwa kusimamia vizuri rasilimali tulizopewa tunaweza kutolewa kwenye usimamizi huo na nafasi hio akapewa mtu mwingine asimamie badala yetu, hapa dipo mwanzo wa malalamiko yataanza, mara ukoloni mara hakuna uzalendo nk.

Tunatakiwa kufikiri na kutumia vizuri rasilimali tulizopewa kwa ajili ya kunufaisha kila mtu. Kwenye maisha huwa hakuna kitu kinaokea na kuwa na madhara makubwa kwa ghafla au kwa mara moja, kila kitu ukiangalia kwa makini utaona kama kimengenezwa. Kwa mfano hakuna sehemu inaweza kuwa jangwa kwa mara moja bila kutengenezwa, hakuna, hakuna sehemu inaweza kuwa na mmon’onyoko wa udongo bila kutengenezwa hakuna vita au migooro inayoanza kwa mara moja gafla huwa inatengenezwa na hatua ndogo ndogo au vitu vidogo vidogo vinavyo fanyika mara kwa mara, hadi baadaye vinakuwa vitu vikubwa na tunashindwa kuvizuia au kuvidhibiti.

Kwa upande mwingine hata mambo mazuri yanayoonekana hayakutokea tu gafla kwa mara moja, kuna hatua na maamuzi mazuri yalifanyika kidogo kidogo kwa muda mrefu, pia hata amani sio kwamba ilikuja tu na kuwepo hapa, hapana, ni juhudi na maamuzi madogo madogo yaliyokuwa yanafanyiwa kazi kila siku. Hivyo basi hakuna kitu kinachotokea tu hapo kwa papo kama vile muujiza, pia wakati mwingine hata muujiza una mchakato wake. Ninachotaka tulelewe leo ni kwamba vitu vidogo vidogo tusividharau hata kidogo vitasababisha madhara makubwa endapo vitaendelea kupewa nafasi ya kufanyika mara kwa mara.

Hivyo ndugu yangu unayesoma na kufuatilia makala hizi nataka nikuahidi kwamba makala hizi zinamanufaa sana, huu ni uwekezaji mdogo mdoo unaoufanya kwenye maisha yako ambao utakuwa na matokeo mazuri sana kwenye maisha ya kazi zako, nchi yako na hata kwa watoto wako, naamini kwa maarifa unayojifunza kila siku kupitia blogu hii yatasaidia wengi, hizi ndio hatua ndogo lakini zenye matokeo makubwa na mazuri kwa jamii na maliasili zetu.

Kwa vyoyote vile tunatakiwa kujifunza mambo ya msingi kwenye maisha na wakati mwinine tunatakiwa kuchukua hatua, pia tunatakiwa kuwapa mkono wa shirika wenzetu wenye maona mazuri na maisha ya baadaye ya nchi yetu kwa kutambua juhudi zao na mioyo yao ya uzalendo katika kuinua taifa letu. Tuanatakiwa kuunga mkono juhudi zozote za kizalendo kwenye nchi yetu, kwa watu binfsi na hata mashirika mbali mbali ya ndani na nje ya nchi.

Nimalizie makala hii kwa kusema na kukumbusha wadau wote wa sekata ya maliasili na utalii pia hata sekta nyingine, wahenga walisema “usipoziba ufa utajenga ukuta”,  hivyo sisi tunatakiwa kuishi na kufanya kazi zetu kwa hekima na busara sana, na endapo tunaoa kitu chochote au maamuzi yoyote yanafanyika au yanataka kufanyika na hayana nia nzuri ya kuhifadhi na kutunza mazingira yetu au rasilimali zetu,  tuchukue hatua mara moja, hatupaswi kukaa kimnya na kuangali mwisho ake utakuaje, wala hatupaswi kabisa kuyalea mambo haya kabisa, hata kama ni jambo dogo kiasi gani macho yetu yanatakiwa kuwa hapo.

Ahsante sana kwa kusoma makala hii.

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

0742092569/0683 862 481

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtalaam.net/wildlifetanzania