Habari msomaji wa makala za wildlife Tanzania, karibu kwenye makala ya leo ambayo tunaendelea kuichambua Sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009. Tukiwa tunaelekea mwishoni mwa uchambuzi wa sheria hii, nataka ujue wanyama na ndege waliotajwa sana kwenye baadha ya sehemu za sheria hii. Wakati tunaanza uchambuzi wa sheria hii kuna vifungu vingi sana vinataja wanyama ambao wapo kwenye majedwali ya sheria hii. Sasa leo tutaona jedwali la kwanza na wanyama waliopo kwenye sehemu hii ya jedwali. Kwenye sheria ya wanyamapori wametumia majina matatu kwa lugha ya Kiswahili, kingereza na jina la kisayansi wakati wa kuwataja wanyama na ndege hawa.
Jina la kiswahili | Jina la kingereza | Jina la Kisayansi |
Babakoko sanje | Sanje Mangabay | Cercocebus sanjei |
Choroa | Oryx | Oryx beisa callotis |
Chui | Leopard | Panthera Padus |
Duma | Cheetah | Acinonyx jubatus |
Faru | Black Rhinoceros | Diceros bicornis |
Kipunji | Highland Mangabey | Lophocebus kipunji |
Mbuzi mawe (Nguru) | Klipsgringer | Oreotragus oreotragus |
Mbwa mwitu | Wild dog | Lycon pictus |
Mindi | Abbotts Duiker | Cephalophus Spadix |
Nyati (Mbogo) | Buffalo | Snycerus caffer caffer |
Nzohe | Sitatunga | Limnotragagus spekeii |
Pahalahala rosaveti | Rosavelt Sable | Hipotragus niger rosalvetii |
Pimbi | Hyrax | Heterohyrax/Procavia |
Pundamilia | Zebra | Equus burchellii |
Sengi | Giant Elephant Shrew | Rynochocyon uduzungwensis |
Sheshe | Puku | Kubus vardoni |
Simba | Lion | Panthera leo |
Simbamangu | Caracal | Felis caracal |
Swala robati | Robart Gazzele | Gazella granti robartsi |
Swalatwiga | Gerenuk | Litocranus walleri |
Tandala mdaogo | Lesser Kudu | Strepsiceros imberbis |
Tembo (Ndovu) | African Elephant | Loxodonta Africana |
Tohe- mlima | Mountain Reedbuck | Redunca fulvorufula |
Korongo nyangumi | Shoebill (Whale headed stock) | Balaeniceps rex |
Korongo usomwekundu | Watle Crane | Bugeranus carunculatus |
Kozi kipanga | Peregrin Falcon | Falco peregrinus |
Kwale uduzungwa | Uduzungwa Forest Patridge | Xenoperdix uduzungwaensis |
Ninga | Green Pigion | Treron |
Mamba | Slender Snorted Crocodile | Crocodilus crataphractus |
Chura wa Kihansi | Kihansi Spray Toad | Nectophrynoides asperginis |
Hivyo Rafiki naamini kabisa utakaposoma makala au seheria wakitaja wanyama waliopo kwenye majedwali basi nadhani utaelewa vizuri kabisa. Leo nimetaja tu wale wanyama na ndege wanaopatikana kwenye Sehemu ya kwanza ya Jedwali na jedwali la kwanza. Karibu kwa maswali na maoni, bila kusahau ushauri.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569