Habari rafiki yangu, tumepotezana kwa siku nyingi sana, lakini naamini bado unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku. Leo baada ya kupotea kutokana na changamoto ambayo ilikuwa nje ya uwezo wangu, nimejitahidi kwa kadri ya uwezo wangu, pia namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa tena nafasi ya kuendelea kuwa pamoja.

Computer yangu ambayo huwa natumia kuandika makala na barua mbali mbali za uhifadhi ilipata changamoto kidogo, hivyo nikaamua kutafuta nyingine ili tuendeleze kazi yetu ya kutoa maarifa ya maliasili zetu na utalii.

Bado kuna mengi ya kufahamu na kujuzana kuhusu maliasili zetu, hivyo usichoke wala kusita kuendelea kujifunza na kufahamu mengi zaidi kuhusu maliasili na utajiri wa Tanzania yetu.

Nakukaribisha, karibu tuendelee kuwa pamoja, kujifunza na kufahamu mengi zaidi.

Ahasante sana!

Hillary Mrosso!

0683 862 481