Habari mpendwa msomaji wetu wa makala za wanyamapori, naamini Mwenyezi Mungu bado anatujalia sote uzima na nguvu za kuendelea kupambana na maisha. Karibu tena darasani kwetu, tuendelee kujifunza zaidi kuhusu wanyamaporina uhifadhi wao kwa ujumla. Naamini unaendelea kujifunza na kupata taarifa sahihi kabisa za wanyama hawa kama ambavyo leo nimekuandalia makala ya maeneo muhimu na yenye utajiri mkubwa wa ndege nchini kwetu. Karibu sana tuanze pamoja na tumalize pamoja.

Picha 1: Hapo juu hao ni heroe wadogo (lesser flamingo) ambao wanategemea zaidi kuzaliana katika ziwa Natron kwa asilimia 90% na huweza kuzaliana idadi yao ikianzia 1000-3000.

Utangulizi; Ukiacha utajiri wa madini na wanyamapori wakubwa uliyopo nchini Tanzania pia ina maeneo mengi muhimu ya ndege na jamii nyingi tofauti za ndege kwa mfano ndege mkubwa zaidi duniani asiye kimbia mbuni pia ndege mkubwa anayeruka angani tandawala mkubwa (kori-bustard). Kwa Afrika mashariki ikishika ngazi ya kwanza ikifatiwa na Kenya, na hivyo ina jumla ya spishi 1000 za ndege ambao 800 ni ndege wa nchini wasio hama na 200 ambao wana tabia ya kusafiri na kurudi. Kati ya hao wote spichi 56 hutambulika katika uhifadhi wa kidunia, 21 kati ya hizo spishi hupatikana Tanzania pekee na 43 ni wale ambao wanakaa nchi moja au mbili tu.

Kutokana na idadi kubwa ya spishi za ndege, ina maeneo mengi ambayo yameainishwa kama makazi ya ndege achana na hawa ambao wanaonekana kwenye makazi ya watu. Tanzania ina maeneo yenye upekee (Endemic Bird Areas) kwa makazi ya ndege ambayo ni milima inayounganisha Tanzania na Malawi ikiundwa na spishi 32 zinazopatikana Tanzania pekee, Msitu wa pwani ya Afrika Mashariki ambayo ina spishi 5 na kisiwa cha Pemba kikiwa na spishi 4 zote zinazopatikana Tanzania tu, milima ya bonde la ufa safu za Albertine ambapo kuna safu za Serengeti zenye spishi 6 za ndege  wa Tanzania pamoja na maeneo owevu makubwa matatu ambayo ni mabwawa ya kusini magharibi, bonde la Kilombero na Magharibi ya ziwa Victoria.

Mpaka sasa maeneo yaliorodheshwa kama maeneo muhimu ya ndege nchini yapata 80, ambayo ni sawa na eneo la mraba 167,000 au 18% ya nchi nzima ambayo pia yanaanzia ukubwa wa hekari 3 mpaka milioni 5 hekari. Na machache nimeyachambua hapo chini.

1.Ziwa Natron; ambalo hupatikana kaskazini mwa Tanzania, 58km kusini mwa mpaka wa Tanzania na Kenya. Ziwa Natron ni ziwa la magadi ambalo ni eneo muhimu kwa mazalia ya heroe mdogo na mwekundu (lesser flamingo) pia upande wa magharibi ya tambalale ya Kilimanjaro milima ya Longido wanapatikana kwa urahisi buff-crested bustard, spike-heeled lark. Pia rahisi kuona jamii za wanyama wengine kiurahisi kama gerenuk, steenbok na tandala wadogo.

2.Miinuko ya Hifadhi ya Taifa ya Kitulo: ambayo ndio hifadhi pekee Afika kwa ujumla iliyoundwa na aina tofauti tofauti za maua hivyo wakati mwingine huitwa “bustani ya Mungu”. Ina ndege wa kipekee amabo ni Denham’s bustard pamoja na Blue swallow.

3.Ziwa Victoria: ambalo hupatikana nchi tatu za Afrika Mashariki, na kwa upande wa Tanzania linatumika sana na ndege maji ambao ni cormorants, yangeyange (egrets),  korongo (herons) na ndege mwingine Spotted-necked Otters ambaye hupatikana na Hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Rubondo.

4.Kisiwa cha Zanzibar: kisiwa hichi kiwa kina spishi mbili za kipekee ambazo ni crab-plovers na Fischer’s Turaco, Greenbul na Grey sunbird ambao hutegemea zaidi hifadhi ya msitu wa Jozani ambao pia ni miongoni mwa misitu ya visiwani wenye ndege wa kipekee. Pia East coast akalat wanapatikana pia na wanyama wengine kama Zanzibar red colobus, Ader’s duiker na Pemba flyimg fox.

5.Kisiwa cha Pemba; kisiwa hichi kiko umbali wa 55km kutoka Tanzania bara na kutunza spishi nne za kipekee ambazo ni Pemba green pigeon, Pemba scops owl, Pemba sunbird na Pemba white-eye.

6.Fukwe za jiji la Dar es salaam: fukwe hizi ambazo zimeundwa na tambalale ya tope la mawimbi ya bahari, pia kama kiunganishi cha maji ya chumvi na baridi kutoka vijito tofauti vya jiji pamoja na misitu ya mikoo hivyo kutoa nafasi kubwa kwa makazi tofauti ya ndege ambapo inajumuisha spishi 450. Pia fukwe hizi muhimu kwa ndege wa masafa miongoni mwao ni waders kama Grey plover, little stint na curlew sandpiper.

6.Hifadhi ya taifa Ruaha: ni miongoni mwa hifadhi kavu nchini ambayo ina jumla ya spishi 560 za ndege, ambapo kati ya hizo spishi mbili hupatikana Tanzania tu ambazo ni Ashy starling na yellow-collared lovebird.

7.Hifadhi ya taifa Serengeti: hifadhi yenye jina kubwa nchini na imeweza pokea tuzo nyingi za kimataifa kama sehemu pekee bora barani Afrika kwa utalii, ikiongezewa sifa na nyumbu wenye misafa ya msimu Tanzania na Kenya. Inapatikana katikati ya ziwa Victoria na bonde la ufa la mashariki karibu na hifadhi ya Masai Mara Kenya na upande mwingine inapakana na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro. Serengeti ina spishi kuu tatu za kipekee ambazo ni Grey-breasted spurfowl, Fischer’s lovebird na Rufous-tailed weaver pia ndege wa masafa marefu kutoka magharibi na ulaya ni rahisi kuwaona katika kipindi chao cha safari.

8.Eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro: hili limeorodheshwa kuwa na jumla ya spishi 500 za ndege ikiwa na makundi makubwa ya Fischer’s lovebirds, pia eneo hili lina mabwawa na ardhi owevu ambayo ni muhimu kwa greater and lesser flamingos, pia rahisi kumuona faru mweusi mnyama ambaye yupo hatarini zaidi kutoweka.

9.Hifadhi ya taifa Mkomazi: hifadhi hii inapakana na safu za mlima wa Pare kusini, na ina ndege tofauti kama Friedmann’s lark, pygmy batis, three-streaked Tchagra, shelley’s starling na Pringle’s Puffback.

10.Hifadhi ya taifa ya milima ya Udzungwa: hifadhi hii ipo upande wa kusini magharibi kutoka jiji la Dar es salaam ambako kuna msitu wa akiba wenye spishi mbali mbali na mara chache kuonekana maeneo ya kawaida ambazo ni Udzungwa partridge, Dappled mountain-robin, Sharpe’s akalat, Olive-flanked robin-chat pamoja na White-chested alethe. Pia hifadhi hii ina maeneo mengi lakini eneo la maporomoko ya maji ya Sanje linavutia na kuipendezesha hifadhi hii.

11.Safu za milima ya Uluguru: ni eneo ambalo lipo kati kati ya jiji la Dar es salaam na Udzungwa, ndo eneo pekee kwa ajili ya Uluguru bush-shrike na Loveridge’s sunbird pamoja na spishi nyingine tano, na mara nyingine inaweza ikatokea bahati kumuona Abbott’s duiker ambaye ni mnyama jamii ya swala na hupatikana  kwa nadra sanaaa nchini.

12.Safu za milima ya Usambara mashariki: eneo hili ni miongoni mwa maenao muhimu Afrika bala kwa uhifadhi wa spishi zinazosumbuliwa  na zenye tishio la kutoweka kidunia. Spishi hizo ni kama Usambara eagle owl, Sokoke scops owl, Long-billed tailorbird, Dappled mountain-robin, Swynnerston’s robin pamoja na Usambara weaver.

13.Misitu ya fukwe za wilaya ya  Lindi: fukwe hizi ni eneo muhimu kwa spishi nyingi za ndege wa misitu ya fukwe kama Southern banded snake eagle, East coast akalat, Spotted ground-thrush pamoja na Livingstone’s flycatcher.

Pamoja na kwamba nchi yetu ina maeneo mengi na jamii nyingi za ndege, bado kuna changamoto nyingi ambazo kwa namna moja au nyingine zinarudisha nyuma uhifadhi wa ndege kiduniana na kitaifa pia. Changamoto hizo ni pamoja na

  • Uelewa mdogo wa utajiri wa kipekee na wa asili wa wanyama pori na ndege tulinao kwenye nchi nyingi za kiafrika,
  • Uharibifu wa mazingira na makazi asili ya wanyama hawa kama ardhi owevu ambako ndege wengi hutumia kuzaliana,
  • Kukua kwa miji na majiji kunako ambatana na ongezeko kubwa la majengo marefu (ghorofa) na nguzo za umeme ambazo zinachangia sana kufa kwa ndege wetu,
  • Kuwindwa kama kitoweo au kwa manyoya yao hasa maeneo ambayo hutumia kupumzika hasa kwa ndege wanaosafiri umbari mrefu kati ya Afrika na Ulaya.

Tunakazi kubwa katika uhifadhi wa wanyama hawa, hasa kwa kuanza kubadilisha mitazamo ya jamii hizi husika za kiafrika kisha kutengeneza njia sahihi za uhifadhi wenye kunufaisha jamii husika na wanyama pori. Na, hapo itakuwa ni hatua nzuri kuelekea uhifadhi bora wenye mafanikio makubwa na changamoto chache zaidi hasa za tabia ya nchi.

Usikubali kuishi pasipo kujifunza vitu vipya, ni dalili moja wapo ya umauti”

Makala hii imetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kutoka Makala ya lugha ya Kingereza “Important Bird Areas in Tanzania”, 25/01/2013 na kuhifadhiwa na African Bird Club.

Asantenii sana

Kutafrisiwa na kuandikwa;

Leena Lulandala

lulandalaleena@gmail.com

 0755369684

Mwanafunzi-UDSM