Habari msomaji wa wildlife Tanzania karibu kwenye makala ya leo ambapo tunaendelea na uchambuzi wa sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009. Nimedhamiria kuweka kila kitu kwenye sheria hii kwa lugha rahisi na nyepesi kwa ajili ya wote wanaopenda kuelewa na kujifunza mambo haya wayaelewe vizuri hata kama hawajui kingereza. Rafiki yangu karibu kwenye makala ya leo tuendelee na uchambuzi wa sheria hii kwenye kipengele cha pili ambacho kinahusu ukamataji wa wanyama au kwa lugha ya kimombo wanaita “capture of Animal” ambapo tutaangalia ukamataji na wa wanyamapori kwa mujibu wa sheria hii.

  1. (1) Isipokuwa vinginevyo imeelezwa na sheria hii, Hakuna mtu atakaye kamata mnyama wa aina yoyote, iwe huyo mnyama ameainishwa kwenye jedwali lolote la sheria hii au hajaainishwa, isipokuwa na kulingana na masharti ya kibali cha ukamataji ambayo kimetolewa kwa mujibu wa sheria hii. Kama ambavyo sheria imesema wazi hakuna ukamataji wowote utakaofaanyika kwa mnyama yoyote aliyetajwa kwenye majedwli yaliyopo kwenye sheria hii bila kibali ambacho kitatolewa kwa mujibu wa sheria hii.

(2) Sawa sawa na mapendekezo ya Sheria hii,Mkurugenzi anaweza kutoa kwa maandishi, kibali cha kukamata mnayama yoyote kwa ajili ya-

(a) kutoa sampuli kwa ajili ya bustani ya zuologia au taasisi inayoendana nayo;

(b) kielimu, kisayansi au kwa kusudi la kitamaduni; na

(c) kutoa sampuli kwa ajili ya masuala ya kibiashara.

(3) Utolewaji wa kibali cha ukamataji kama ilivyoelezwa kwenye kifungu kidogo cha (2) inatakiwa kufanyika kwa ajili ya maslahi ya umma na inatakiwa iwe sawa na mapendekezo yoyote ya kimataifa ambayo yamekubaliwa na kuungwa mkono na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  1. Mkurugenzi anaweza kutoa kibali cha ukamataji, baada ya Waziri kuafiki na pia kwa kuzingatia masharti na kanuni za ukamataji, uangaliaji, kulisha, sehemu ya kulala, kusafirisha na kusafirisha nje ya nchi wanyama kama ilivyo tajwa kwenye kanuni.
  2. (1) kibali cha uwindaji kinatakiwa kielezewe kwenye fomu ambayo inataja mnyama na eneo ambalo ndani yake mnyama huyo anaweza kukamatwa.

(2) Kibali cha ukamataji wanyama kitakuwa halali mpaka muda ambao Mkurugenzi atauelezea.

(3) Kutakuwa na ada ambayo itatozwa ambayo itakuwa ni kwa mujibu wa kibali cha ukamataji ambacho Waziri anaweza baada ya kutoa taarifa kwenye Gazeti la serikali, kuielezea au kuamuru.

(4) kulingana na mapendekezo ya kifungu kidogo (3), mtu yeyote au mamlaka ya serikali mtaa, watatozwa tozo ya kicheo au tozo cha hadhi kulingana na kibali cha uwindaji.

Ukamataji wa wanyama kinyume na sheria (Unlawful capture of animal)

Katika kifungu hiki cha sheria kinaelezea ukamataji wa wanyamapori kinyume na sheria.

53.- (1) Mtu yeyote ambaye-

(a) sio mmiliki wa kibali cha uakamtaji, kukamata mnyama yeyote;

(b) ambaye ni mmiliki wa kibali cha ukamataji, kukamata-

(i) aina au maelezo ya spishi ya mnyama tofauti na aliyeainishwa au kutajwa kwenye kibali; au

(ii) idadi kubwa ya wanyama kuliko iliyoruhusiwa na kibali; au

(iii) mnyama katika eneo ambalo ni tofauti na eneo ambalo limetajwa kwenye kibali,

anafanya kosa na atakuwa na hatia-

(aa) kwa kesi ambayo inahusu kuwa na hatia kutokana na kukamata mnyama aliyetajwa katika Sehemu ya I ya Jedwali la Kwanza la Sheria hii, atahukumiwa kwenda jela kwa kifungo kisichopungua miaka mitatu lakini kisizidi miaka mitano na pia mahakama inaweza kumwongezea adhabu ya kulipa faini isiyopungua mara mbili ya thamani ya mnyama aliyekamatwa.

(bb) kwa kesi ambayo inahusisha kuwa na hatia kwa kukamata mnyama ambaye ametajwa kwenye Sehemu ya II ya Jedwali la Kwanza la Sheria hii, atahukumiwa kwenda jela kwa kifungo kisichopungua miaka miwili lakini kisizidi miaka mitano na mahakama inaweza kumwongezea adhabu ya kulipa faini isiyopungua mara mbili ya thamani ya mnyama aliyekamatwa;

(cc) kwa kesi ya kuwa na hatia inayohusisha kuakamata mnyama ambaye ametajwa kwenye Sehemu ya III ya Jedwali la Kwanza ya sheria hii, atahukimiwa kwenda jela kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili lakini kisizidi miaka mitatu, na pia mahakama inaweza kukuongezea adhabu ya kulipa faini isiyopungua mara mbili ya thamani ya mnyama aliyekamatwa; au

(dd) kwa kesi ya kuwa na hatia inayohusu kumjeruhi mnyama katika wakati wa kumkamata, atawajibika kulipa faini isiyopungua mara mbili ya thamani ya mnyama aliyejeruhiwa au kuhukumiwa kifungo jela kisichopungua miezi mitano lakini kisichozidi miezi kumi na mbili.

Hivyo msomaji na Rafiki yangu naamini kufikia hapa tumepata mwanga mzuri wa kuelewa kipengele hiki cha pili ambacho kipo kwenye sehemu ya Saba ya sheria hii ya wanyamapori. Endelea kufuatilia na kujifunza mambo ya kisheria kwenye makala hii kuhusu wanyamapori na maliasili nyingine.

Mwisho, tukutane Kesho kwa makala nyingine nzuri hapahapa kwenye matandao wako wa wildlife Tanzania.

Ahsante sana!

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 248 681/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania