Duniani kuna wanyama jamii ya swala aina 90 ambapo bara la Afrika peke zipo jamii 71. Swala wanapatikana marneo mbali mbali duniani ikiwemo Africa na Bara la Asia.

Kutokana na kuwa na aina nyngi za wanyama jamii ya Swala,  watu wengi wamekuwa wanashindwa kutofautisha majina yao Hii ni kutokana na kwamba wanyama hawa  wanafanana muonekano. Pamoaja na hilo ipo tofauti kubwa kwa swala kimaumbo, rangi, tabia na namna wanavyoishi. 

Mnyama aina ya Korogo katika hifadhi ya Taifa Burigi-Chato (Picha na Alphonce Msigwa)

 Lakini pia majina ya kisayansi ya swala yamekuwa tofauti kwa Sababu swala wametawanyika Sana katika maeneo mbali mbali duniani (high diversity). Kutoka na mtawanyiko huo, baadhi ya majina ya swala yametokana na tabia au sehemu wanazopatikana.

 Swala wana sifa za aina mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine ndio imepelekea kuwa na aina hizi 90 duniani kote. Kupitia makala hii, utajifunza sifa mbalimbali za wanyama hawa jamii ya swala.

  • Swala ni wanyama ambao chakula chao kikubwa ni nyasi. Hivyo hufanana na wanyama wa kufugwa kama vile Mbuzi na Kondoo
  • Wanyama jamii ya swala wana uwezo wa kukimbia kwa kasi sana
  • Wanyama hawa hawawezi kuweka miili yao sawia (Balance) wanapokimbia. Hii ni kutokana na urefu wa miguu yao
  • Swala wanachenga nyingi sana wanapokimbia hivyo kusabsbishwa wasikamatwe kwa urahsi na wanayama wanaokula nyama kama vile Simba, Duma na fisi.
  • Wanyama hawa wana uwezo mzuri wa kuruka juu japokuwa hawana uwezo wa kupanda miti kutokana na umbile la miguu yao yaani kuwa na kwato.
  • Pembe za wanyama hawa hujitoa ngozi kila mwaka ili kuweza kukua vizuri na kufanya wawe na muonekano tofauti tofauti kutoka aina moja na nyingine
  • Jamii ya Swala ambaye ana mapembe yaliyojikunja( andika chanzo cha hii picha)
  • Swala wanaishi katika makundi au ngome ambayo inaongozwa na dume. Dume mmoja anaweza kuwa na majike hadi sabini.Ili kuogoza kundi, madume ni lazima wapigane na mshindi ndio ataongoza kundi.
Swala pala katika hifadhi ya Taifa Burigi-Chato(Picha na Alphonce Msigwa)

  • Swala wanauwezo mkubwa wa kunusa  na kuona pia  (visual and smell acute) ambayo  huwasaidia kujilinda dhidi ya  maadui
  • Wanyama hawa huwasiliana kwa njia sauti ambayo hutolewa kama ishara pale mmoja wapo anapomuona adau au hatari
  • Wanyama hawa wana manyoya laini mazito na yenye rangi nzuri inayowasaidia kujificha dhidi ya maadui. Pia ngozi zao buwasaidia kujikinga na jua Kali au baridi kutokana na kuwa na mafuta mengi
  • Pembe za wanyama hawa zina mikuno inayosadia wakati wa kujitoa ngozi na kuwatofautisha baina ya jamii moja na nyingine
Jamii ya swala wenye manyoya mengi na ya kuvutia aina ya Kuro

  • Swalama wanapatikana maeneo ya wazi, nyasi au miti mirefu pia kando ya sehemu zenye maji maji(wetland). Hii huwasaidia pia kujikinga dhidi ya maadui zao, , mfano ukienda mbuga nyingi hapa nchini TANZANIA swala ni rahisi Sana kumuona kuliko wanyama wengine  wakubwa  mfano hifadhi za Taifa za Mikumi, Serengeti, Saadani, na mapori ya kiba kama Kilombero nk.

 Jamii ya Swala wanaopatikana Tanzania

Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa  kuwa na swala wa aina nyingi na wanaopatikana katika mapori ya akiba na hifadhi za taifa nyingi . Baadhi ya Swala hao ni pamoja na sitatunga (nzohe) puku, swalapala nyumbu, Pofu, kudu,  Kuro, Tohe, swala granti, Taya,

1.Pichani: sheshe(puku) katika bonde la hifadhi ya Kilombero

Nzohe( sitatunga) ndani ya Moyowosi.

Nyumbu(wanapatikana katika mbuga na mapori ya akiba mbalimbali nchini)

Uwepo wa wanyama hawa nchini Tanzania ni faida kubwa kwani baadhi hupatikani katika nchi hii tu, mfano sitatunga (nzohe). Hivyo  sisi kamawahifadhi na watanzania wote tunahaki ya kulinda na kuwatunza dhidi ya ujangili ili wasipotee kwani wanyama jamii ya swala huonekani , kwa urahisi katika kipindi tunapofanya utalii na kupelekea kuwa maarufu  na chanzo kikubwa cha mapato nchini.

Asanteni sana kwa kusoma makala hii iliyoandaliwa na.

 KAMANGA SHADRACK ANDREA

Email bigstarshadrack@gmail.com

Mawasiliano 0678577786

Na kuhaririwa na Alphonce Msigwa-Mwikolojia Hifadhi za Taifa Tanzania

Shares:
  • Felipe Palazzolo
    August 5, 2021 at 3:08 pm

    Hi! I could have sworn I’ve been to this site before but after browsing through many of the articles I realized it’s new to me. Anyhow, I’m certainly pleased I came across it and I’ll be bookmarking it and checking back frequently!

    Reply
  • Leopoldo Henningsen
    August 7, 2021 at 1:24 pm

    Having read this I believed it was rather enlightening. I appreciate you finding the time and energy to put this article together. I once again find myself personally spending a significant amount of time both reading and leaving comments. But so what, it was still worth it!

    Reply
    • Hillary Thomas Mrosso
      August 16, 2021 at 11:39 pm

      Great, thank you Leopold for this appreciation feedback, it mean a lot to us and every one reading your comments, and feel free to comments and pass to many other coming articles.

      Reply
  • […] Makala nyingine kuhusu wanyama jamii ya swala unaweza kusoma hapa.Zijue Sifa Za Wanyama Jamii Ya Swala […]

    Reply
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *