Habari msomaji wa Wildlife Tanzania, karibu kwenye makala ya leo ambayo tunakumbushana kuhusu ile ofa kabambe iliyotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA mnamo tarehe 28/7/2017. Ofa hii ya kutembelea hifadhi za taifa ilitolewa kwenye kipindi hiki cha sikukuu za nane nane ambapo zinafanyika Dodoma zinaelekea ukingoni kabisa. Kwa namna ya kipekee nikukumbushe kuwa nafasi bado zipo kwa ajili ya wale wanaopanga kutembelea hifadhi za Tarangire na Ruaha.
Kwa mujibu wa tangazo lao wataanza kupeleka wakazi wa Dodoma kuanzia tarehe 28/07/2017 hadi 07/08/2017. Kwa maelezo zaidi unaweza kutembelea banda la Maliasili na Utalii, huko Nanenane Dodoma.
Leo nimepanga kutokuandika makala ndefu kwa ajili ya jambo lolote ila nataka kukukumbusha usiiache nafasi hii, ni ya kipekee na ni muhimu kwako kutembelea hifadhi hizi. Unajua mambo huwa hayajirudii mara kwa mara, unaweza ukaenda Tareangire au Ruaha kwa ofa hizi lakini unaweza kusiwepo na ofa za kurudia kwenda Tarangire na Ruaha tena, hivyo wanaweza kwenda hifadhi nyingine zaidi ya hiyo, labda Katavi, Gombe au Rubondo.
Hivyo mkazi wa Dodoma tumia muda huu kushiriki safari hii ya kitalii ambayo itakuwezesha kuona vivutio mbali mbali kwa macho yako mwenyewe.
Kumbuka mtu mzima anachangia 60,000
Watoto wanachangia shilingi 40,000 umri kuanzia (5-16)
Gharama hizi zitajumlisha malazi, mwongoza wageni, na kiingilio na gharama za usafiri. Hivyo utajigharamia kwa chakula na vinywaji. Kuna makala nimeelezea kwa kina safari hii.
Pia ikumbukwe hii ni ofa kwa ajili ya watanzania tu. USISAHAU KUBEBA KAMERA YAKO!
Asanteni sana, karibuni hifadhini
Hillary mrosso
Wildlife Conservationist
+255742092569/ +25568248681