Habari ndugu wasomaji wa makala za blogu yetu ya WILDLIFE TANZANIA.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa kuwa wasomaji wazuri wa makala zetu tunazoandika kuhusu wanyamapori, mazingira, uhifadhi na utalii.

Mara zote mmekuwa mkitupa nguvu na sababu ya kuona tunachokifanya kina maana sana kwa jamii na uhifadhi wetu kwa ujumla.

Nawashukuru sana wale waliotushauri, kututia moyo, kutoa maoni mbali mbali kuhusu kazi yetu ya uandishi wa makala hizi.

Kuandika makala sio kazi rahisi, lakini tunafanya hivyo ili kutoa elimu kwa jamii yetu kuhusu uhifadhi na utalii wa maliasili zetu.

Tunatamani kila mtu ajue umuhimu wa kila kiumbe hai na mazingira yake katika uhifadhi, ili kwa pamoja tuwe na uelewa wa kuhifadhi maliasili zetu.

Tunawashukuru wadau wote waliosapoti kazi hii ya uandishi pamoja na kulipia gharama za hosting na domain za blog hii. Kwa weli wamefanya kazi nzuri na tunawashukuru sana kwa moyo wao mzuri wa kujitolea kwenye jambo hili.

Kwasasa blog yetu inatambulika kama www.wildlifetanzania.or.tz  na sio ile ya mwanzo isiyokuwa na usajili wala domain name. Makala zote na kazi zote za uandishi zitakuwa zinapatikana kwenye hii blog.

Nawashukuru Chuo Kikuu cha Kilomo cha Sokoine, Idara ya Usimamizi wa wanyamapori kwa kutambua mchango wetu katika uandishi wa makala hizi za kuelimisha jamii kuhusu uhifadhi na wanyamapori. Jambo hili limeongeza ari na juhudi ya kuendelea kuandika makala bora za kuelimisha jamii kuhusu uhifadhi na wanyamapori.

Nawashukuru waandishi wote waliovutiwa na kazi hii ya uandishi na kuandika makala zao, nawapongeza sana kwa moyo wao na juhudi kubwa waliyoonyesha katika uandishi wa makala bora sana za uhifadhi.

Baadhi ya Makala za mwaka 2023, unaweza kuzisoma hapa.

Monica Mahilane, Monica aliandika makala kadhaa za kuelimisha na kutoa elimu muhimu sana ya uhifadhi kwa jamii, moja ya makala yake unaweza kuisoma hapa. Mimea Vamizi Tishio kubwa Katika Maeneo ya Hifadhi  za Wanyamapori

Sadiki Kashuku, Sadick ameandika makala nyingi sana kwenye hii blogu, moja ya makala zake za hivi karibuni ni kuhusu mnyama aina ya swala, wengi wetu hatumjui mnyama huyu, unaweza kusoma makala yote hapa. Asilimia 97 Hawamjui Huyu Mnyama Jamii ya Swala

Cecilia Mwashihava, Cecilia ni mwandishi, ameandika makala kadha za kuelimisha na kuhimiza watu kuhamasika kufanya utalii, moja wapo ya makala yake ya hivi karibuni unaweza kuisoma hapa. Yajue Maajabu Ya Ziwa Ngozi Nchini Tanzania

Leena Lulandala, Leena ameandika makala nyingi kwenye blog hii, moja ya makala yake ya hivi karibuni unaweza kuisoma hapa. Zijue Sababu Saba (7) Zinazopelekea Migogoro Baina ya Binadamu na Wanyamapori Kutoisha

 

Ezra Peter Mremi, Ezra ni mwandishi na mtafiti mzuri, ameandika makala muhimu sana kuhusu popo na mamba, unaweza kusoma moja ya makala yake ya hivi karibuni kuhusu mamba. Unajua Nini Kuhusu Mamba? Haya ni Mambo Usiyoyajua kabisa kuhusu Mnyama Mamba

Ester Matingisa, huyu ni mtalaamu wa ndege Tanzania, anawajua ndege wengi sana hata kwa sauti, unaweza kuona makala yake hapa.Zifahamu Tabia za Spishi za Ndege Wanaohama Kutoka Nchi Moja Kwenda Nchi Nyingine

Leon Hermenegild, wengi hatufahamu mengi kuhusu nyuki, katika makala hii Leon, ametuandalia mambo yote muhimu tunayotakiwa kujua kuhusu nyuki na umuhimu wake, fahamu mengi kuhusu nyuki kwa kusoma makala hii. Mfahamu Nyuki Na Umuhimu Wake Kiuchumi na Kiikolojia

Marylove Shoo, huyu dada anawajua wadudu , ni mtalaamu wa wadudu kama siafu mchwa nk, alituandikia makala bora sana kuhusu wadudu na umuhimu wake kwenye uhifadhi, unaweza kusoma hapa kufahamu zaidi. Hizi Ndio Faida za Wadudu Kijamii na Kiikolojia

Maureen Francis Daffa, huyu dada anapenda sana ikolojia ya bahari na maji, anapenda viumbe wa baharini, alituandikia makala bora sana kuhusu viumbe wa baharini, unaweza kusoma makala hiyo hapaUsiyoyajua Kuhusu Matumbawe, Hazina Yenye Thamani Chini Ya Bahari

Victor Obadia Wilson, huyu ndugu anapenda sana uhifadhi wa bahari na majini, anapenda sana ikolojia ya mambo ya bahari, hivyo alituandikia makala muhimu sana kuhusu mimea ya baharini inayoitwa MWANI, unaujua mwani wewe? Soma makala hiyo hapa kufahamu mengi zaidi kuhusu mwani.Faida za Kilimo cha Mwani na Athari Zake Katika Uhifadhi wa Bahari

Alphonce Msigwa, Alphonce ni mtafiti mzoefu kwenye masuala yanayohusiana na mazingira, wanyamapori na binadamu kwa zaidi ya miaka kumi na saba.  Amefanya kazi na mashirika ya kitaifa na kimataifa ikiwemo taasisi za serikali kama vile Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokione katika miradi ambayo inajihusisha na uchunguzi wa kina juu ya magonjwa yanayoweza kuambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu. Kwa sasa ni mwikolojia wa hifadhi za Taifa Tanzania, Mratibu wa mradi wa Katavi-Mahale & Corirdor (KAMACO) na afisa usalama wa mazingira wa mradi wa kuimarisha usimamizi wa maliasili na kukuza utalii kusini mwa Tanzania (REGROW). Unaweza kusoma makala yake hapa.Magonjwa Manne Hatari Zaidi kwa Watumiaji wa Nyamapori

Martin Bayo, Bayo ni mhifadhi na mtafiti mwenye uzoefu mwingi, ameandika makala nzuri sana kuhusu fisi maji, wengi wetu hatuwajui Fisi maji, kupitia makala hii, tutajifunza mambo muhimu yaliyoandikwa kuhusu mnyama huyu.Mambo Ya Kushangaza Usiyoyajua Kuhusu Mnyama Aina Ya Fisimaji

Amos. B. George, Amosi ameandika makala nzuri sana kuhusu Reptilia, amewachambua na kuweka sifa zao, kuna mengi unaweza kujifunza kwenye makala hii iliyoandikwa na Amos, tafadhali isome hapa. Mambo Usiyoyajua Kuhusu Tofauti Zilizopo Kati Ya Nyoka Aina Ya Cobra(Fira/Swila) Na Black Mamba(Koboko)

Shadrack Andrea Kamanga, ndugu yetu Shadrack alituandikia makala nzuri sana kuhusu umuhimu wa ndege kwenye ikolojia, unaweza kusoma makala yake hapa kufahamu mengi.Fahamu Umuhimu Wa Ndege Kama Kiashiria Cha Hali Ya Mifumo Ya Ikologia Katika Maeneo Mbali Mbali

Naomi Mnyali, Naomi ni mwandishi mzuri wa makala za wanyamapori, ameandika makala kadhaa, ambazo zinatoa elimu muhimu sana kwenye uhifadhi na jamii kwa ujumla, unaweza kusoma moja ya kazi yake hapa.Mfahamu Kwa Kina Maisha Ya Kiumbe Asiye Na Kidole Gumba

Lucia Levelian Romward, Lucia ni mwandishi na mwanaharakati katika uhifadhi, ameandika makala kadhaa za kutoa elimu kwa jamii kuhusu uhifadhi wa wanyamapori, unaweza kuona moja ya makala yake hapa.Mfahamu Ndege Bundi, Tabia Zake Na Uhalisia Kuhusu Bundi

Hillary Mrosso, Hillary ni mmiliki wa blogu hii, ameandika makala nyingi sana, moja wapo ya makala zake ni hii. Spishi za Kakakuona wa Tanzania, na Mengi Usiyoyajua kuhusu Wanyama Haw

Hizi ni baadhi tu ya kazi za uandishi zilizofanywa na waandishi hawa, tunafanya kazi hii ya uandishi bila malipo yoyote, nia nyetu ni kuona tunatoa elimu ya kutosha ili watu, wanyama, ndege, wadudu, samaki na mimea iendelee kuwepo hapa duniani kwa miaka mingi ijayo, lakini pia viumbe wote tuweze kuishi hapa duniani bila kuleta madhara kwe viumbe wengine.

Mwisho, napenda kuwashukuru wote wanaosoma na kuwashirikisha wengine makala hizi, mnafanya kazi nzuri pamoja nasi. Tuendelee kujifunza na kufuatilia makaala za blogu hii ili kujifunza pamoja.

Nawatakia Kheri na Baraka za mwaka Mpya 2024.

Hillary Mrosso