Karibu kwenye blog ya WILDLIFE TANZANIA.

Huu ni mtandao ambao utakupa taarifa na maarifa kuhusu maliasili na hifadhi za taifa zilizopo nchini Tanzania.

Kupitia mtandao huu utaweza kunufaika na yafuatayo;

  1. Kupata elimu na maarifa muhimu yatakayosaidia kuwa na uwanja mkubwa kufanya maamuzi mazuri kwenye maeneo ya uhifadhi na usimamizi wa wanyamapori, utalii na jinsi jamii inavyoweza kunufaika na uwepo wa  wanyamapori kwenye maeneo yao.
  1. Kujifunza kwa njia rahisi ili kila Mtanzania na mtu mwingine yeyote aelewe misingi na manufaa ya uwepo wa hifadhi za Taifa pamoja na kushiriki kikamilifu kwenye uhifadhi wa mazingira halisi ya maliasili zetu.
  1. Kujenga tabia za kizalendo kwa watanzania ili tuwe na utamaduni wa kutembelea hifadhi zetu na pia kushiriki katika uchangiaji wa pato la nchi kupitia utalii wa ndani.
  1. Kwa wanafunzi na watu wenye ndoto ya kufanya kazi kwenye maliasili yeyote, kama hifadhi au kuanzisha biashara za kitalii basi hapa ndipo utapata maarifa muhimu ya kukuongoza.
  1. Pia kupitia blog hii tutajifunza fursa ambazo zinapatikana kwenye hifadhi zetu na hata kwenye mapori ya wanyamapori na sehemu nyingine zinazoweza kuwa kivutio kwa watalii.

Karibu Mtanzania mwenzangu ili tuweze kujenga na kuendeleza  maliasili zetu kwa kizazi cha sasa na cha baadaye, huu ni wajibu wetu sote tunaishi kwenye nyakati na majira haya, fanya kitu kwenye kizazi chako kwa ajili ya kuweka misingi imara na mizuri kwa kizazi kijacho. Asante sana!